Hali ya siasa nchini ni ya hamasa, lakini isiyokuwa na misingi endelevu.
Kwa kuwa Rais amekuwa akigawa fedha wakati chombo cha kufanya hivyo kipo ambacho ni bunge.
Pia nasononeshwa ninapoona watu wanaachishwa kazi na mashirika mbalimbali kwasababu ya hali ngumu ya uendeshaji wa mashirika hayo.
Bandari sasa hivi nasikia uingizaji mizigo umeshuka kwa asilimia 50, kampuni nyingi za mizigo zimefunga shughuli zake na pale palikua na vijana wetu wengi wameajiriwa,sasa hivi wako mtaani hakuna mbadala wa ajira, hii inasababisha hali ya maisha ya wananchi yanakua magumu.
Kuhusu swala la MCC ni pigo kwa mustakabali wa uchumi, kutaka nchi ya viwanda kunahitaji uwekezaji mkubwa,katika hili fedha tutatoa wapi kama sio wafadhili wa ndani na nje kufanikisha?
Hawa wafadhili sio watu wa kuwabeza kwakuwa tunafanya nao miradi mingi ya kimaendeleo na wanavyotoka hivi itaturudisha nyuma, Tunahitaji kujitegemea, ndiyo, ila kwa mipango huku tunatafuta mbadala wa kila msaada.
Hapa kinachotakiwa ni kufanya mabadiliko katika mfumo na kuufanya kuwa endelevu.
HAHAHAHAHAHAH!BABU HEBU TEKELEZA AHADI YAKO YA KWENDA KUCHUNGA NG'OMBE KWANZA.
ReplyDeleteWewe lowassa ni fisadi tungekupa nchi hii ungetuibia ndio maana unatetea mafisadi kuachishwa kazi. Rudi kijijini kwako hachana na mambo ya siasa huiwezi, hakuna atakaekuchagua mwaka 2020
ReplyDeleteBabu muache atukomeshe tu yeye si anaona sifa anunue ndege aandikwe kwenye magazeti wakati huku kwa wananchi hali mbaya na anajua.,achatukome babu itafika zamu yake atakuja kuomba kula ndo atagundua yuko mwenyewe hata mama samia atamtoroka,endeleza sifa tu huku uchumi unashuka nunua meli ndege treni alafu apande yeye na mkewe maana mlo mmoja hatuwezi ku afford nauli ya meli tutatoa wapi
ReplyDeleteSana mdau, asituharibie nchi. Bora aende huko akachunge ngombe, wengi hawana mpango na wewe,umejaa michosho tu ya wizi na kifisadi, tupishe kuleeee
ReplyDeleteYaani hadi kichefu chefu kwa hayo anayoyasema, watu wamechoka na hao mafisadi, na wezi, maanake ndio hao wanaolipekea Taifa hili kwenye umasikini wao wanaishi vizuri maisha ya kifahari. Na watanzania wengine wanaishi maisha ya kimasikini, loooo huyu angepita, Tanzania ingekuwa kwishinei
ReplyDeleteHUNA LOLOTE KACHUNGE NG'OMBE WAKO UFISADI TU UMEKUJAA
ReplyDeleteyah usemayo ni kweli tupu EL
ReplyDeletemagazetini nao ndio kila siku wao na rais na rais na magazeti ndio kazi iliyobaki mngepunguza mkasubiri yenye tija ndio muandike,.. au ndo mnauza kwa jina lake.. mwe manyumbu! utaona kichwa cha habari MAJIPU MAGUFULI TUMBUA. habari ni MAJIPU tu. du!
ReplyDelete