Lugumi yazua Balaa Lingine..Maofisa wa Polisi Wahaha Kuunganisha Mitambo ya Alama za Vidole ifanyaje Kazi

Sakata la mkataba kati ya Jeshi la Polisi Tanzania na Kampuni ya Lugumi Enterprises wa kufunga vifaa 108 vya kuchukua alama za vidole katika vituo vya polisi, limezua balaa lingine kufuatia madai kwamba, maofisa wa polisi wameanza kupita katika vituo wilayani na mikoani kukagua na kuunganisha mitambo hiyo ili iweze kufanya kazi.

Taarifa zilizopatikana kutoka ndani ya jeshi  hilo zinadai kuwa, zoezi hilo limeanza huku kukiwa na usiri mkubwa.

Habari kutoka makao makuu ya polisi zinasema kuwa, maofisa wa polisi walitawanywa vituo mbalimbali nchini wakifuatilia kwa karibu suala hilo ambalo linalitikisa vichwa vya viongozi serikalini.

Aidha, gazeti hili likiwa Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Pwani, Ijumaa iliyopita lilishuhudia maofisa wa polisi wakiwa na wataalam kutoka makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar na kuambiwa walikwenda kwalengo la kuunganisha mashine hizo ili zianze kufanya kazi.

Baadhi ya polisi kituoni hapo waliozungumza kwa masharti ya kutotajwa majina kwa kuwa siyo wasemaji, walidai kuwa kutofanya kazi kwa mashine hizo kulizorotesha shughuli za upelelezi hasa namna ya kuwatafuta wahalifu sugu wanaofanya uhalifu mkoa mmoja na kuhamia mwingine bila kujulikana.

Wakifafanua umuhimu wa mitambo hiyo, polisi hao walisema mhalifu, hasa jambazi anapokamatwa katika kituo chochote cha polisi, akifikishwa wilayani au mkoani hupigwa picha na kuchukuliwa alama za vidole na kuingizwa katika mtandao, hivyo kuwa rahisi kujua kama alishawahi kufanya uhalifu popote nchini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, ACP Bonaventura Mshongi alipoulizwa kama amepokea ugeni wa polisi kutoka makao makuu kwa ajili ya kufuatilia mashine hizo, alikiri kupata wageni ofisini kwake. Hata hivyo, hakuwa tayari kufafanua walichokifuata.

Tayari bunge limeunda kamati ndogo yenye wabunge tisa iliyopewa kazi ya kuchunguza kwa kina mkataba huo, kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Aeshi Hilary.

Hilary alisema kuundwa kwa kamati hiyo kumetokana na uamuzi wa Spika wa Bunge, Job Ndugai ambaye ameielekeza kwenda kuchunguza kwa kina mkataba huo na kupewa siku 30 za kufanya kazi hiyo kisha taarifa itatolewa bungeni.

Kamati hiyo itawahoji mawaziri, viongozi wa jeshi la polisi waliopo na waliostaafu na wafanyabiashara waliotajwa pamoja na kampuni zilizoshiriki kufunga mashine hizo.

Naye Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai (DCI), Diwani Athuman alipotafutwa kwa njia ya simu na Uwazi, juzi (Jumapili), alisema hana taarifa hizo na badala yake akaelekeza atafutwe msemaji wa jeshi la polisi, Advera Bulimba ambaye mpaka gazeti hili linakwenda mitamboni, hakupatikana.

Mwaka 2011, Kampuni ya Lugumi  ilipewa zabuni ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya polisi 108 nchini ambapo inadaiwa imeshalipwa Sh. bilioni 34 kati ya bilioni 37, sawa na asilimia 99 ya malipo yote.

Hata hivyo, kuna madai kwamba ni vituo 14 tu vilivyofungwa mashine hizo huku mashine moja pekee ikiwa ndiyo inayofanya kazi.

Chanzo:GPL

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hivyo teknolojia inavyobadilika kola siku..mashine za mwaka 2011 is now obsolete.. Rudisheni Fedha za Polisi halafu tunakupelekeni mahakamani mnalipa fidia na hizo stock mashine badala ya kuzidistroy tutapeleka msaada huko Nchini Burundi au Swaziland.. Na cc tutatoa tends nyingine za alama ya macho( Eye Scan) ambazo Ni uhakika zaidi na tecknolojia ya Tanzania yet mpya chino ya Mh. Kassi Majaliwa na Baba JPJM...WADAU AMA SIVYO.. FIGURE PRINT IMESHAPITWA NA WAKATI.. MIAKA YA AWAMU NZIMA YA UONGOZI ..TUMESHINDWA KUTEKELEZA HAYA

    ReplyDelete
  2. Ndo CCM mpya, Ndo Polisi ambao Taifa linawategemea. Ndo usalama wa Taifa la Nchi yetu. Je Ndugu magufuli, ni nani mhusika mkuu wa haya majipu ya CCM. Ni uongozi mzima wa CCM ni mbovu. Na kama ni mbovu, CCM haiaminiki. Mnaingiaga kazini kwa speed, mnawahujumu Watanzania, Mnakuja na mpya kutumbua. Utamtumbua Raisi aliyepita ndiye yeye aliyeshindwa hii kazi. Ndiye yeye aliyewapa huru Wana CCM kulihujumu Taifa na hawezi kukwepa. Wakati Wapinzani wakisema tumbua majipu halisi tunaelewa. Kuanzia ngazi ya juu bila hivi unapapasa majani tu. Taifa liko mikononi mwako, uwe Shupavu, wafanyie haki Watanzania. Rudisha mali za Watanzania walizogawana kiurafiki, kifamilia na madudu ya nje waliojipenyeza Tanzania kwa miaka hii kumi baada ya kuua Azimio la Arusha kama asemavyo kabwe. Viongozi wa Taifa wana maslahi binafsi kupitia vyeo vyao. Conflict of Interest for God sake. Watawatumikiaje mabwana wawili sawa kwa wakati mmoja. Raisi wa awamu ya nne ameshindwa sababu kuu hiyo.Kwa nini msipeane ukweli. Kama huwezi kutoa ukweli basi usiwe Raisi wa kupapasa. Waacheni wenye ushujaa na uchungu wa Watanzania na Tanzania waongoze nchi badala ya kuziba watu macho mkijua majipu makubwa yanaranda na kutamba duniani kila kukicha.Unahitaji Hekima, Akili, Elimu sai, Sushuri na mwisho uchaji wa Mungu. Msimkejeli Mungu. Mnajikejeli wenyewe.Rudisha nguvu ya uchumi kwa Watanzania wanaofanya kazi usiku na mchana na kubanwa na watu wenye nguvu kisiasa, kupitia wizi bila sababu.
    Nakuomba soma haya ujitafakari upya kupitia sheria safi ambazo zinahitaji katiba mpya kwanza. Kupitia sheria tu, utawatendea haki Watanzania na si ubabe. Sababu sheria zikiwa wazi itakuwa ni rahisi na uhuru utakuwepo. Lete Katiba na sheria kali kusudi Watanzania wote washiriki sawa kuikomboa nchi yao. Hapa utajenga ukuta safi , imara, na wakudumu.

    ReplyDelete
  3. MAGU HAPA NDO KIPIMO CHAKO KWA LUGUMI NA BAADHI YA MAWAZIRI WAKO ULIOTEUA WAPO WANAHUSIKA LAKINI UMEPIGA KIMYA KWA KUTAFUTA UMAARUFU WA KISIASA

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad