Lulu juzikati alitupia ujumbe mtandaoni akimjibu mmoja wa mashabiki wake aliyeuliza sababu ya yeye na mama Kanumba kutoiva ambapo aliandika:
“…ni hivi mimi siyo chizi jamani kila ninachokifanya nakijua vizuri tu, mimi ndo’ najua ‘what’s going inside’ (nini kinachoendelea) nyinyi wa nje yasikieni hivyohivyo, sitajibu watu wala mhusika mwenyewe ila siku ikifika nitaongea.”
Baada ya kupostiwa kwa ujumbe huo, mashabiki walimjia juu Lulu wakieleza kuwa, hana sababu ya kumtisha mama Kanumba badala yake kama kuna lililo moyoni mwake aliseme kuliko kukaa kimya.
“Huku sasa ni kumtisha mama wa watu, kama analo jambo aliseme watu wajue sababu ya bifu lao,” alisema mmoja wa mashabiki.
Baada ya kulipata hilo paparazi wetu alimtafuta mama Kanumba na kumuuliza juu ya maneno hayo yaliyotafsiriwa kuwa ni ya vitisho kwake ambapo alifunguka:
“Namshangaa sana huyu mtoto, ana siri gani nzito baina yangu mimi na yeye, sina siri naye huenda anataka kutoa siri ya kifo cha mwanangu aitoe basi, tena aitoe haraka hiyo siri wala asisubiri hiyo siku ifike.
“Tena itakuwa vizuri akiita vyombo vya habari na kuianika kama ni kubwa hivyo au aniite aniambie, nimemuacha na maisha yake ananifuatafuata sitaki kabisa.”Kwa upande wake Lulu alipotafutwa kuzungumzia ishu hiyo alijibu kwa kifupi; “Nimeshasema sitaki kuongea na mtu yeyote kwa sasa, tena wewe mwandishi ‘nimeshaku-block’ nashangaa unanipigia kwa namba nyingine.”
Chanzo:GPL
Picha ndo limeanza sasa....daah...mtoto huyu haya yetu macho
ReplyDeleteLulu wala usihitaji kujibizana na mama Kanumba yeye mwenyewe mama Kanumba anajua Kanumba alikuwa Freemason, siku yake ya kufa ilikuwa imefika.
ReplyDeleteLulu umeshakua mwanangu, nakuomba upunguze vijimambo visivyokua na faida katika maisha yako. Kumbuka wewe ndie unaejua sababu za kifo cha kanumba na unaejibizana nae ni mama wa marehemu, unapojibizana nae kwa njia ambazo si nzuri kama hizi huwa inaleta hisia tofauti kwa mzazi aliyepoteza mwanae. Hivyo jaribu kujirekebisha ili amani na utulivu ichukue nafasi ndani ya mioyo yenu.
ReplyDelete