Maalim Seif Sharif Hamad |
Kauli hiyo aliitoa jana mjini Unguja, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, baada ya kutangazwa kwa maazimio 13 ya kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho, kilichokutana kuanzia Aprili 2, mwaka huu.
Akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua kama atakwenda Ikulu pindi akiitwa na Dk. Shein kwa ajili ya mazungumzo ya kutafuta mwafaka, Maalim Seif aliweka wazi kwamba hana haja ya kufanya hivyo kwani tangu awali kiongozi huyo hakuwa na nia njema na suala la Zanzibar.
“Siko tayari kukutana na Shein, kama nani na nazungumza nini nikikutana na Dk. Shein Ikulu? Labda kama nitakutana naye kwa njia nyingine sawa za kibinaadamu, lakini hatuko tayari tena kuzungumza na Shein,” alisisitiza Maalim Seif.Alisema haoni uwezekano wa Serikali ya Dk. Shein kuendelea kuwapo madarakani hadi ifikapo 2020 na hilo linatokana na msukumo wa nchi wafadhili kusita kutoa misaada katika baadhi ya miradi waliyoahidi kwa Tanzania.
“Uwezekano wa Serikali hii kuendelea hadi 2020 siuoni kutokana na presha hii ya jumuiya za Kimataifa,” alisema Maalim Seif.