Madereva Wakaidi Agizo la Serikali la Kutopitisha Magari yenye Uzito Mkubwa Kigamboni

Siku cheche baada ya Serikali kuzindua daraja jipya la Kigamboni jiji  Dar es Salaam na kukataza Magari yenye uzito zaidi ya tani kumi kutopita katika daraja hilo baadhi ya madereva wasiofuata sheria wamekuwa wakikiuka agizo hilo nakuonekana kupita katika daraja hilo.

Akitekeleza majukumu yake Inspekta Hassan Amadi ambaye ni mkuu wa usalama barabani wilaya kipolisi Kigamboni amesema kwamba ifike kipindi madereva waache kuvunja sheria na kufuata maelekezo nakuwataka madereva wengine wanaovunja sheria sehemu mbali mbali  hususani wanao tumia daraja hilo kufuata sheria zilizowekwa na kuepuka  makosa kama hayo.

Naye dereva aliyevunja sharia akijaribu kujitetea amesema kwamba hkufahamu utaratibu mzima wa upitaji katika barabara hiyo hivyo anakiri kosa alilofanya nakuwasihi madereva wenzake wafuate  sheria Barabarani.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. WANYANGANYWE LESENI HAVAI KUWA DEREVA KWANI HAONI ALAMA ZA BARABARANI. SI KUNA KIBAO CHA MWISHO TANI KUMI???????????

    ReplyDelete
  2. MMMH SASAIVI HILO DARAJA LITAVUNJIKA

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad