Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni!, japo huyu mama ametumbuliwa, sababu za utumbuzi huo, ni kitu kinaitwa "personal matter", and has nothing to do na utendaji wake TIC, ifike mahali Watanzania tuwe na shukrani kwa mazuri aliyoyatenda.
Mimi kama mwanahabari huru ninayejitegemea, nimeifanyia TIC kazi za kihabari, tangu enzi za TIC ya Samuel Sitta, TIC ya Ole Naiko na hii TIC ya sasa ya Julliet Kairuki, mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 3 tuu ya Juliet Kairuki, ni mara mia ya mafanikio yote yaliyopatikana katika kipindi cha Samweli Sitta na Ole Naiko put together!, hivyo huyu mama pamoja na hilo tatizo lake "personal" la mshahara, amekifanyia makubwa Kituo cha Uwekezaji, na kulifanyia makubwa taifa hili, kiasi cha kuifanya Tanzania kuwa ndio nchi inayoongoza kwa kuvutia wawekezaji kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, kitendo ambacho ni cha kustahili pongezi na kuenziwa na sio kubezwa kama hivi anavyobezwa sasa as if she did nothing!.
Wiki hii nilialikwa katika kipindi cha 360 cha Clouds TV, kuzungumzia uhuru wa habari Tanzania. Swali la mwisho nililoulizwa niliulizwa nitoe maoni yangu kuhusu utendaji wa Rais Dr. John Pombe Magufuli, nilimpongeza Magufuli, na kuzipongeza hatua za utumbuaji majipu kuwa anafanya kitu sasa katika muda sahihi ila njia anayoitumia kutumbulia haya majipu, sio njia sahihi. (Magufuli is doing the right thing, at the right time but in a wrong way), nadhani kwa vile Magufuli ni rais, no ones tells him, kuwa that is not the right way!. Nikasema kwa vile Magufuli ni rais wetu, Watanzania na dunia wana very high regards on him na very high expectations on him, that he has to be perfect, not only on doing the right thing at the right time, but he got to do it right!. Kwa vile maamuzi yake ndio the highest, the king is always right hivyo haya na tuyaache turidi kwenye mada iliyopo mezani.
Kituo cha Uwekezaji Rasilimali Tanzania (TIC) ni Idara inayojitegemea ya Serikali iliyoundwa kwa mujibu wa Sheria ya Uwekezaji Na. 26, ya mwaka 1997 kwa lengo la kuhamasisha na kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje ili kukuza sekta binafsi na hatimaye kuinua uchumi wa Taifa na pia kuishauri serikali juu ya maswala yanayohusu uwekezaji. Kituo kinatekeleza majukumu yake kwa kuongozwa na Bodi ya Wakurugenzi yenye wajumbe sita wanaoongzwa na Mwenyekiti anayeteuliwa na Mhe. Rais. Wajumbe wa Bodi wanateuliwa na Waziri mwenye dhamana ya uwekezaji, aidha Mkurugenzi Mtendaji ambaye naye huteuliwa na Mheshimiwa Rais ni Katibu wa Bodi ya wakurugenzi na pia ni Mtendaji na Msimamizi Mkuu wa shughuli za TIC akisaidiwa na Wakuu wa Idara .
Kituo cha Uwekezaji rasilimali kina makao makuu yake Dar es Salaam na kina ofisi za kanda tatu ambazo zinaongozwa na Mameneja. Kanda hizo ni Kanda ya Kaskazini (Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga) ofisi ziko Kilimanjaro; Kanda ya Ziwa (Mwanza, Shinyanga, Kagera, Mara na Kigoma) ofisi siko Mwanza; na Kanda ya Nyanda za juu Kusini (Mbeya, Iringa, Rukwa, Katavi na Ruvuma) ofisi ziko Mbeya. Kituo kina Idara nne ambazo ni : Utafiti na Mfumo wa Habari, Uhamasishaji Uwekezaji, Huduma kwa wawekezaji, Fedha na Utawala, na masuala ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi ambapo kwa sasa kitengo kimehamia Ofisi ya Waziri Mkuu.
MAJUKUMU YA TIC
TIC inatekeleza majukumu ya msingi yafuatayo:
Kubuni mbinu za kujenga mazingira bora ya uwekezaji nchini Kwa lengo la kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje.
Kuwasaidia wawekezaji kupata vibali na hati mbalimbali za kisheria ili waweze kuwekeza hapa nchini.
Kuandaa na kusambaza taarifa sahihi kwa wawekezaji kuhusu fursa za uwekezaji pamoja na upatikanaji wa mitaji na wabia.
Kushirikiana na Serikali kutafuta maeneo yenye ardhi inayofaa kuwekeza kwa ajili ya wawekezaji.
Kuwasaidia wajasiriamali wadogo na wa kati kuibua fursa za uwekezaji kwa lengo la kukuza biashara zao na kuongeza kipato.
Kuwahamasisha wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza kwenye sekta muhimu zitakazokuza uchumi kwa haraka
Kuwajengea uwezo wafanyakazi wa Kituo ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
UHAMASISHAJI UWEKEZAJI
Kituo chetu cha Uwekezaji kwa kushirikiana na Ofisi zetu za Ubalozi zilizoko nje ya nchi, ziliweza kuandaa shughuli mbalimbali za Kuhamasisha uwekezaji katika nchini mbalimbali Duniani kama ifuatavyo;-
Makongamano ya Kuhamasisha Uwekezaji nje ya nchi
Serikali kupitia ofisi za Balozi zetu zilizoko nje ya nchi na kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji (TIC) tuliweza kushiriki kwenye Makongano yaliyofanyika nchi mbalimbali Duniani ambayo yalitoa nafasi kwa nchi yetu kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini. Baadhi ya nchi ambazo tuliweza kushiriki na kupata fursa ya kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo nchini ni kama vile Marekani, uingereza, China , Japan, Uturuki, India, Afrika ya Kusini, Ethiopia, Sweden, UAE, Thailanda, Singapore, Vietnum, Srilanka.
Kuitangaza nchi yetu nje (Country Branding)
Serikali kupitia Kituo cha Uwekezaji kwa kushirikiana na Shirika la Multichoice (Tanzania) Limited, tuliweza kuandaa sherehe za kutoa tuzo maalum ya CNN kwa mara ya kwanza hapa nchini inayoitwa ‘‘CNN African Journalist Award of the Year’’, kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam. Uwepo wa mashirika makubwa ya utangazaji Duniani kama ilivyokuwa kwa Shirika la utangazaji la CNN wakati wa sherehe hizo ,imewezesha nchi yetu iweze kufahamika Duniani kote kupitia sherehe hizo za utoaji tuzo maalum kwa waandishi wa habari.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe hizo ambazo ziliweza kuhudhuriwa na washiriki kutoka zaidi ya nchi 40.
Ziara za wafanyabiashara wa Tanzania nje ya nchi
Serikali kupitia Kituo cha Uwekezaji iliweza kuandaa ziara za wafanyabiashara wa ndani kwenda nje ya nchi ili kutafuta wabia wa kufanya nao biashara, kutafuta masoko ya kuuzia bidhaa zao, kutafuta teknolojia kwa ajili ya biashara za pamoja na mikopo.
Baadhi ya nchi ambazo ziara hizo zilifanyika ni kama vile Afrika ya Kusini, Kuwait, Bahrain, Oman, Saudi Arabia, Uingereza, Japani, Korea ya Kusini, Brazil, marekani, Canada, UAE, Ujerymani, Italia, China, na Kenya.
Ziara za wafanyabiashara wa nje nchini
Serikali kwa kupitia Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kiamataifa, Ofisi za Balozi za nje zilizoko nchini pamoja na Kituo cha kwekezaji, tuliweza kuandaa ziara za wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchi mbalimbali kuweza kuja nchini kwa ajili ya kujionea wenyewe fursa mbalimbali za uwekezaji zilizoko nchini.Wakiwa nchini, makundi hayo ya wawekezaji na wafanyabiashara waliweza kupata fursa ya kukutana na Kampuni za Kitanzania pamoja na taasisi mbalimbali za Serikali ambazo zilikuwa na miradi ya uwekezaji. Baadhi ya taasisi ambazo walipata fursa ya kukutana nazo ni pamoja na Mamlaka ya Bandari (TPA), Mamlaka ya Viwanja vya ndege (TAA), Shirika la Ndege Tanzania (AIR Tanzania Ltd), Shirika la Kusambaza Umeme nchini (TANESCO), Taasisi ya Umeme Vijijini (REA), Wizara ya Miundo Mbinu, SACOT Centre, n.k.
Makundi hayo ya wawekezaji yalitoka katika nchi mbalimbali Duniani kama vile Marekani, Uingereza, Ubelgiji, Italia, Afrika ya Kusini, India, China, Japani, Vietnum, Singapore, Canada, Brazil, Misri, Israel, Uturuki,Indonesia, , Ujerumani, Denmark, Syria, China, Finland.
Mikutano ya Kimataifa ya Kuhamasisha Uwekezaji iliyofanyika nje ya nchi.
Serikali pia iliweza kushiriki katika mikutano mikubwa ya Uwekezaji Duniani ambayo ilifanyika katika nchi mbalimbali ikiwa na lengo la kutangaza fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji zilizoko nchini. Baadhi ya nchi ambazo Serikali kupitia Kituo cha Uwekezaji iliweza kushiriki ni kama vile Uswizi, Austaralia, Afrika ya Kusini ,Nigeria ambako mkutano wa World economic Forum ulifanyika, nchi zingine ni UAE, Japan, China,na Marekani
Mikutano ya Kuhamasisha Uwekezaji iliyofanyika nchini
Mikutano ,mikubwa ya kuhamasisha uwekezaji imekuwa ikifanyika nchini pia. Mikutano hiyo imekuwa na lengo la kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji zilizoko nchini kwa wawekezaji wa nje na ndani. Serikali imekuwa na utaratibu wa kuandaa mikutano mikubwa ambayo inakuwa na tija kwa Taifa kwa kuzingatia sekta muhimu za uchumi kulingana na vipaumbembele ambavyo tumejiwekea.
Baadhi ya mikutano iliyoandaliwa ni kama vile mkutano uliolenga sekta ya kilimo, chini ya mpango wa ‘‘Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania’’, yaani SAGCOT, chini ya mpango huu wawekezaji wanahamasishwa kuwekeza kulima mashamba makubwa kwenye ukanda wa SAGCOT, mashamba ambayo yatazungukwa na mashamba ya wakulima wadogo wadogo yaani ‘‘outgrowers’’. Mpango huu unatarajiwa kupunguza umaskini kwenye maeneo ya ukanda wa SAGCOT kwa kuwa wakulima wataweza kulima mazao ambayo yatanunuliwa na wawekezaji wakubwa kwenye ukanda huo.
Mikutano mingine iliyoandaliwa ni ile iliyolenga kuhamasisha uwekezaji kwenye sekta ya utalii, sekta ya madini, sekta ya utafutaji mafuta na gesi.
Uhamasishaji Uwekezaji wa ndani
Serikali imekuwa na mkakati mahususi wa kuhakikisha kuwa watanzania wanafahamu fursa za uwekezaji zilizopo nchini na wanafahamu jinsi Serikali inavyosaidia kukuza uwekezaji kupitia taratibu mabalimbali ambazo zimerahisisha mchakato wa kuanzisha miradi ya uwekezaji nchini pia vivutio vya kodi ambavyo vinatolewa kwa wawekezaji wa ndani. Shughuli hizi za uhamasishaji uwekezaji wa ndani zimefanyika kupitia makongamano ya kimkoa, kikanda, mafunzo maalum ya uwekezaji na ujasiriamali kwa wajasiriamali wa ndani, pamoja na kushiriki maonyesho ambayo yamekuwa yakifanyika nchini.
Makongamano ya Uwekezaji yaliyofanyika nchini
Serikali kupia Mikoa na kwa kushirikiana na Kituo cha uwekezaji, imeweza kuandaa makongamano ya uwekezaji yaliyohudhuriwa na watu zaidi ya 2000 kwenye mikoa mbalimbali nchini ikiwemo mikoa ya Mtwara, Ruvuma, Rukwa, Mara,Manyara, Mwanza,Tabora, na Kigoma. Pia makongamano hayo yaliandaliwa katika ngazi ya kanda kama ifuatavyo;-
Kanda ya Kaskazini ambayo inajumuisha mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga - ambapo mkataba baina wa wakuu wa mikoa 4 waliingia makubaliano na Gavana wa Anjouan wa ushirikiano katika biashara na uwekezaji.
Kanda ya nyanda za juu Kusini ambayo inajumuisha mikoa ya Mbeya, Njombe na Iringa.
Kanda ya Ziwa Tanganyika ambayo inajumuisha mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma pamoja na
Kanda ya Ziwa ambayo inajumuisha mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Geita na Kagera - ambapo zaidi yawashiriki 1200 walihudhuria na TIC iliweza kusaini mikataba 6 na wakuu wa mikoa na mkataba mmoja na NARCO kuhusu kutangaza fursa za uwekezaji katika ukanda huo.
Mafunzo ya Uwekezaji na Ujasiriamali yaliyofanyika nchini
Serikali kupitia kituo cha Uwekezaji nchini, kiliweza kuendesha mafunzo kwa wajasiriamali na wafanyabiashara walioko katika mikoa mbalimbali nchini, ili kuweza kuwahamasisha kuanzisha miradi mbalimbali ya uwekezaji na pia kuwajulisha fursa mbalimbali za uwekezaji zilizoko katika maeneo yao na namna Serikali inavyoweza kuwasaidia katika uanzishaji wa kampuni hizo pamoja na unafuu wa kodi ambao Serikali utawapatia kupitia Kituo cha Uwekezaji.
Mafunzo haya ya Uwekezaji na Uwezeshaji yaliweza kuwasaidia sana wafanyabiashara wazawa kwa kuwapatia elimu juu ya maswala mabalimbali yanayohusu uwekezaji nchini, hivyo yamesaidia kuondoa dhana potovu kuwa Serikali imeunda Kituo cha uwekezaji kwa ajili ya kuwasaidia wawekezaji wan je.
Kupitia mafunzo haya, wafanyabiashara wa Tanzania waliweza kupata elimu juu ya kodi mbalimbali wanazopaswa kuzilipa kutokana na kuendesha shughuli zao, namna ya kupata fedha kutoka kwenye vyombo vya fedha n.k.
Mafunzo haya yamefanyika katika wilaya za Mbinga, Songea, Iringa mjini, Singida, Mbozi, Musoma (ikijumuisha Wilaya zote za Mkoa wa Mara),Kilombetro, Ifakara, Kilosa, Ruaha, Makambako pamoja na Njombe.
Kutoa elimu ya Uwekezaji kwa wananchi kupitia Maonyesho.
Kituo cha Uwekezaji kiliweza kushiriki kwenye maonyesho mbalimbali yaliyofanyika nchini kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi kuhusu Kituo cha Uwekezaji kinavyofanya kazi zake na na namna mwananchi wa kawaida anavyoweza kunufaika na shughuli za Kituo cha Uwekezaji. Kituo cha Uwekezaji kiliweza kushiriki maonyesho yanayofanyika kila mwaka kama vile maonyesho ya Sherehe za Saba saba, Nane nane, Maonyesho ya utalii ya Karibu pamoja na maonyesho ya wiki ya Utumishi wa Umma.
Mafanikio ya ziara za Kuhamasisha Uwekezaji wa kutoka nje na ndani.
Juhudi za Serikali za kuhamasisha Uwekezaji nchini zimeweza kuzaa matunda kutokana na ongezeko kubwa la miradi ambayo imeanzishwa nchini kwenye sekta mbalimbali za uchumi wa nchi yetu, miradi hii imeweza kuleta ajira, kuongeza mapato ya Serikali, kuleta teknojia mpya, kuongeza uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za viwandani n.k . Miradi hii kwa kiasi kikubwa imeongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wan chi yetu.
Kulingana na takwimu za Ripoti za Uwekezaji Duniani (World Investment Report) zinazoandaliwa na shirika la UNCTAD, Tanzania imeweza kuvutia miradi mingi kutoka nje (FDI) kuliko nchi nyingine zilizo kwenye ukanda huu wa Afrika ya Mashariki. Mwaka 2005 Tanzania ilivutia mitaji kutoka nje yenye thamani ya Dola za kimarekani ziapatazo 447.6 Milioni. Kiasi hiki kiliweza kuongezeka kwa kasi hadi kufikia kiasi cha Dola za Kimarekani zipatazo 1,872.4 Milioni kwa mwaka 2013.
Uhamasishaji uwekezaji katika ukanda maalum wa SAGCOT
TIC imeendelea kushiriki vikao vya ubia vya SAGCOT ili kuongeza ufanisi katika kuhudumia wawekezaji katika ukanda wa juu kusini. Pia kituo kinaendelea kusimamia mchakato wa uhuishaji wa mashamba makubwa ya Mkulazi lenye ukubwa wa hekta 63,227 kwa ajili ya kupata wawekezaji mahiri wa Kilimo cha Miwa na Mpunga. Wawekezaji wakubwa wapatao kumi (10) walionyesha nia na kuandika michanganuo yao ya biashara katika kuendeleza mashamba. Kati ya hao 7 wameonysha nia kwenye Miwa, 2 katika mpunga na 1 katika mpunga na miwa. Baada ya mchakato wa zabuni kumalizika ni mzabuni mmjoja tu ndio aliyewakilisha mchanganuo wake na baada ya kamati kuipitia haukukuwa umefikia vigezo vinavyotakiwa.
HUDUMA KWA WAWEKEZAJI WA NDANI NA NJE
Usajili wa Miradi ya Uwekezaji (2005 -2014)
Kwa kipindi cha Mwaka 2005 hadi 2014, Kituo cha uwekezaji kimesajili jumla ya miradi 7159, miradi ilikadiriwa kuwa yenye thamani ya dola za Kimarekani zipatazo 154,274.5. Miradi hii ilikusudiwa kutoa fursa za ajira kwa watanzania wapatao 969,464
Sekta iliyoongoza kwa idadi ya miradi ni Uzalishaji/Usindikaji viwandani, ikifuatiwa na sekta ya Utalii na Usafirisha na Majengo ya Biashara. Angalia Kielezo namba 1 hapa chini
Katika kipindi cha mwaka 2005 hadi mwaka 2014 kati ya miradi 7159 iliyosajiliwa, miradi 3,535 sawa na asilimia 49.38 ni miradi ya wawekezaji wa ndani, miradi 1,676 sawa na asilimia 23.41 ni miradi ya Wawekezaji wa Kigeni, na miradi 1946 sawa na asilimia 27.18 in miradi ya ubia baina ya Watanzania na wageni kutoka nchi za kigeni. Usajili huu wa miradi mingi ya watanzania ni mafanikio makubwa kwa sababu:
Kwanza lengo serikali katika kukuza uwekezaji ni kutaka watanzania waingie na kumiliki uchumi wa nchi hii na hii ni dalili mojawapo.
Pili malengo serikali ni kuhamasisha uwekezaji wenye tija kwa watanzania hasa kwa kuwapa hajira zitakazowawezesha kukuza uzalishaji na kupata kipato.
Tatu Kuwekezwa kwa mitaji hiyo ni kichocheo katika uzalishaji wa bidhaa na huduma katika kiuchumi wa nchi na inaleta tija kwa taifa kwa kuongeza wigo wa kulipa kodi. Zikiunganishwa na ajira inakuwa na tija katika kuingiza technolojia na utaalamu ambavyo uboresha huduma na bidhaa kuweza kuingia kwenye masoko ya kisasa ndani na nje ya nchi na hivyo kubadilisha maisha ya watanzania kama Ilan ya chama cha mapinduzi inavyosema “MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA”.
Katika kipindi hiki chote cha mwaka 2005 – hadi mwka 2014 Kupungua kwa miradi katika kipindi chamwka 2009 – 2010 na mwaka mwaka 2014 kumesababishwa na mabadiliko ya sheria ya kodi kwa Wawekezaji katika bidhaa za mtaji(deemed capital goods) ambayo yalianza kutekelezwa kuanzia mwaka wa Fedha 2008/2009 mpaka miaka ya hivi karibuni
Utoaji huduma za vibali na leseni mbalimbali kwa wawekezaji chini ya mfumo wa “One Stop Shop”.
Katika kipindi cha cha 2005 hadi 2014 Kituo kimeendelea na maboresho katika kuhudumia wawekezaji ili kupata vibali mbalimbali kwa haraka wakati wa utekelezaji na uendeshaji wa miradi. Katika maboresho hayo Wizara ya Kazi na Idara ya Uhamiaji imeteua maofisa kuidhinisha vibali hivyo kwa niaba ya Makamishna wa Kazi na Uhamiaji. Mpango wa baadae ni kuhakikisha kuwa huduma nyingine zote zikiwepo za Kodi, ardhi, kufungua kampuni n.k zinatolewa ndani ya TIC kwa mfumo huo hapo juu nakuanza kutumia mitandao ili kurahisisha utoaji wa vibali.
Katika kipindi husika kitengo cha ardhi kiliendelea kutoa huduma za ushauri kwa wawekezaji katika masuala mbalimbali ya ardhi pamoja na kuainisha maeneo yenye ardhi kwa ajili ya uwekezaji katika maeneo mbalimbali ya Tanzania. Kitengo cha Ardhi Kilifanikiwa kilishughulikia jumla ya maombi 15,969 ya kumilikishwa ardhi, na jumla ya hati zisizo asili Derivatives /Leasehold title 39 zimekamilika na kukabidhiwa wawekezaji.
Katika kitengo usajili wa makampuni jumla ya maombi ya Makampuni 1246 ziliweza kuandikishwa kwa kutumia ofisa wa BRELA aliyepo hapa Kituoni.
Kitengo cha leseni za biashara kilifanikiwa kutoa jumla ya leseni za biashara 1034 kwa ajili ya ashughuli mbali mbali za wawekezaji.
Kitengo cha Kazi (Labour) na Uhamiaji walifanikiwa kuwapatia vibali vya daraja A kwa ajili ya wenye hisa na daraja B kwa ajili ya wafanyakazi, jumla ya vibali 26,535 vilitolewa katika kipindi hicho.
Kitengo cha TRA kilifanikiwa kuhudumia jumla ya wateja 35,783 kwa kuwasaidia kupata huduma kama vile, misamaha ya kodi, usajili wa mlipa kodi na VAT, na maswala mbalili yahusiyo kodi kwa ujumla.
Kuunganisha Wafanyabiashara Wadogo (SMEs) na Makumpuni Makubwa
Tangu programu ya kuwaunganisha wafanyabiashara wadogo na wa kati na wawekezaji wakubwa ianzishwe mwaka 2009 kituo kimeweza kutoa mafunzo ya wafanyabisahara (SMEs) 451 ambapo wanaume walikuwa 275 na wanawake 176. Mafunzo hayo yanayochukua siku sita (6) kwa kozi na yameweza kufanyika Dar es Salaam, Mbeya ikishirikisha mikoa ya ukanda wa juu Kusini, Moshi, Tanga ikishirikisha mikoa ya ukanda wa Kaskazini na Mwanza ikishirikisha mikoa ya Kanda ya Ziwa. Mafunzo hayo yana lengo la kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wajasiriamali wadogo kwa lengo la kuwajengea uwezo kwa jinsi ya kubadili mitazamo hasi, kuongeza utaalamu katika kutoa huduma au bidhaa, na kutunza mahesabu na kuboresha mahusiano ya kibiashara (Business Linkage) na makampuni makubwa katika sekta za mawasiliano, ujenzi, kilimo, saruji, madini, viwanda vya samaki, Viwanda vya Usindikaji Maziwa Viwanda vya bia, Viwanda vya vinywaji baridi na hoteli. Katika kipindi husika Jumla ya wafanyabiashara/ wasambazaji wa bidhaa na huduma wa ndani (local suppliers) 81 walihitimu mafunzo hayo.
Aidha tangu programu ya Business Linkages ianzishwe hapa Kituoni kwa kushirikiana na UNCTAD mafanikio mengi yamepatikana kwa kutoa mafunzo na kuwaunganisha wajasiriamali wapatao 150 kwa makampuni makubwa 20 kama kiambatanisho kinachofuata kinavyoonyesha
Huduma kwa Wawekezaji Waliopo (After-care Services)
Kituo kilitembelea miradi mbali mbali ya wawekezaji na kutoa huduma bora (Aftercare Services) ili kujenga mahusiano mazuri na wawekezaji, kutatua matatizo yao na kujenga mazingira mazuri ya uwekezaji. Katika kipindi husika katika jitihada za kutoa huduma kwa wawekezaji kwa malengo ya kutatua kero zinazokabili miradi na pia kushauri wawekezaji kupanua miradi ili kuongeza mitaji na ajira kwa Watanzania. Changamoto zilizoainishwa katika kutembelea miradi hiyo ni pamoja na;
Uchelewezwaji wa vibali mbalimbali vya kuwasaidia wawekezaji kuendeleza miradi yao
Miundombinu ya barabara na bandari
Umeme usio wa uhakika
Gharama kubwa za mafuta ya kuendeshea mitambo
Mlolongo mrefu wa kupata Ardhi kwa ajlili ya upanuzi wa miradi
Mabadiliko ya mara kwa mara ya punguzo la kodi katika vifaa vya mtaji (deemed capital goods/ incentives)
Uagizwaji mazao ya kilimo na mbegu kutoka nje unaathiri soko la ndani
Ufanisi duni kutoka katika bodi za mazao
Uhamasishaji Miradi ya Wawekezaji Mahiri (Strategic Investors)
Katika jitihada za kuhamasisha uwekezaji wa kimkakati, TIC imesajili jumla ya miradi mikubwa ya kimkakati 45. Miradi hiyo inatarajia kuwekeza kiasi cha dola za Marekani bilioni 8.4
Miradi inayohusisha sekta mbalimbali, ambazo ni kilimo, viwanda, nishati, usafirishaji, utangazaji, miundombinu na mawasiliano.
Miradi katika sekta ya kilimo imechukua asilimia 39, viwanda vikubwa asilimia 26, miundombinu asilimia 16, nishati asilimia tano, usafirishaji asilimia tano, utangazaji asilimia tatu, maliasili asilimia tatu na mawasiliano asilimia tatu.
UTAFITI NA UBORESHWAJI WA MAZINGIRA YA BIASHARA
Tafiti za Uwekezaji
Tafiti za kiuwekezaji zilizofanyika zililenga kusahidia kufahamisha na kushauri serikali juu ya mambo yanayoendelea kwenye uwekezaji ili maamuzi sahihi yafanyike katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na pia kuibua fursa za uwekezaji na kurahisisha kazi ya kuinadi nchi ndani na nje kiuwekezaji.
Utafiti wa mitaji ya kutoka Nje - Foreign Direct Investment
Katika vipindi vyote viwili, serikali iliwezesha,TIC kwa kushikiana na Benki Kuu ya Tanzania pamoja na Ofisi ya Takwimu ya Taifa kukamilisha tafiti ya tano (5) za ufuatiliaji wa wa uwekezaji wa miradi ya kigeni hapa nchini (makampuni yenye mitaji kutoka Nje) zijulikanazo kama Tanzania Investment Report (TIR)ambayo huonesha mwenendo wa uwekezaji wa kigeni hapa nchini. Taarifa hiyo huzalishwa karibu kila mwaka na takwimu zake huchangia pia katika ripoti ya uwekezaji ya dunia.
Lengo la tafiti hizo ni kufuatilia uwekezaji wa sekta binafsi unaofanya na mitaji iliyotoka nje ya nchi, hasa kwa kujua wanawekeza kutoka nchi gani, kiasi gani, sehemu gani, katika sekta gani, wanafanya nini na wanahusianaje na wenyeji (watanzania).Tafiti hizo zinafaida nyingi kwa taifa letu:
Kwa kujua nchi inakotokea mitaji hiyo, sera za mahusiano kati ya nchi yetu na nchi hizo hutengenezwa na kuimarishwa.
Kwa kuongea na wawekezaji wa mitaji hiyo serikali imeweza kugundua changamoto na vikwazo wanavyokumbana navyo na hivyo kuweka mikakati ya kuboresha mazingira ya uwekezaji.
Kujua sekta ambazo mitaji hiyo imewekezwa kumesahidia serikali kujuwa maeneo ya kuvutia wawekezaji na hivyo kuweka juhudi zaidi katika kuimarisha taarifa za fursa za uwekezaji na miundombinu ya maeneo hayo.
Baadhi ya matokeo ya utafiti unaonyesha kuwa;
Mitaji kutoka nje iliongezeka kwa wastani wa 10.3% (kutoka dola za kimarekani milioni 7,751.0 hadi 10,393.2)
Uwekezaji katika shughuli za umeme na gesi uliongezeka kwa kasi kubwa katika kipindi cha utafiti kwa mwaka 2008 hadi 2011 ambapo uwekezaji ulikuwa na thamani chini ya dola za kimarekani milioni 3.0 kwa mwaka 2008 na 2009, uliongezeka hadi kufikia dol aza kimarekani milioni 290.5 mwaka 2010 na dola za kimarekani milioni 209.4 mwaka 2011.
Sehemu kubwa ya faida iliyopatikana iliwekezwa nchini kwa wastani wa 82.5% (2008 hadi 2011) hii inaonyesha wawekezaji kuwa na imani na serikali na mazingira ya uwekezaji kwa kipindi cha utafiti.
Mtazamo wa wawekezaji na Uhusiano na Uchumi wa Ndani (Investors Perceptions) wakilinganisha walivyoanza biashara na wakati utafiti ulipofanyika ulionyesha kuwa;
Kulikuwa na uboreshwaji wa mazingira ya uwekezaji hasa katika huduma za benki, mawasiliano, uhamiaji, usafiri wa anga na nchi kavu.
Umeme usiokuwa wa uhakika ulibakia kuwa ni changamoto kwa wawekezaji
Shughuli za uzalishaji viwandani na kilimo ziliongoza katika utoaji wa ajira ambapo asilimia 94.1 ya waajiriwa ni wazawa na asilimia 5.9 ni wageni.
Makampuni mengi yalikuwa na mipango ya kuongeza uwekezaji hapa nchini ambapo 75.7% yalionyesha kuwa na mipango ya kuongeza uwekezaji kipindi cha miaka mitatu ijayo. Aidha 19.9% yalionyesha kutokuongeza uwekezaji na 4.4% yalionyesha yatapunguza kiwango cha uwekezaji. Mtazamo huu unaashiria kuwa wawekezaji wameridhishwa na jitihada za serikali za kuboresha mazingira ya uwekezaji hapa nchini.
Mtiririko wa mitaji kutoka Nje (Foreign Direct Investment)
Tanzania imeendelea kuongoza katika kuvutia wawekezaji kutoka nje ikilinganishwa na nchi nyingine katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa takriban miaka sita mfululizo kuanzia mwaka 2008. Takwimu zinaonyesha thamani ya FDI imeongezeka kutoka dola za kimarekani milioni 1,706 (2012) mpaka dola za kimarekani milioni 1,872 (2013) ambapo ni sawa na ongezeko la 9.7% Ongezeko hili limechangiwa zaidi na sekta ya mafuta na gesi katika miaka ya karibuni.
Soko la Ajira na madhara yake kwa fursa za uwekezaji nchini “A study of Labour Market and Impacts on Investment Opportunities in Tanzania” ambao ulilenga kupitia takwimu za ajira kupitia uwekezaji, kuchunguza mambo muhimu katika ajira ya Tanzania (ukubwa wa ajira, uwezo wake, utaalamu). Pia kuchunguza matatizo ya soko la ajira kwa kutoa picha halisi ya mwenendo wa ajira nchini na kushauri jinsi ya kuongeza ufanisi au kushauri juu ya njia mwafaka ya kuyatatua.
Madhara ya umeme kwa uwekezaji “A report on Power crisis in Tanzania and Its Impact on Investment” uliolenga kushauri juu ya changamoto za umeme kwenye uwekezaji hasa gharama na kutoaminika katika kupatikana (Tarriffs and unreliable supply)
Uwezo na Mlinganyo wa Tanzania kwa mataifa mengine juu ya uwekezaji “Tanzania’s Competitive and Comparative Advantages”. Utafiti huu ulilenga kuweka wazi uwezo wa Tanzania ukilinganishwa na nchi nyingine duniani ili kusaidia kuvutia uwekezaji zaidi.
Ukuwaji wa uwekezaji na matokea ya uwekezaji huo kwa nchi “Report on the Study of growth and Impact of Investment in Tanzania” ulilenga Kupima kazi zinazofanywa na kituo katika kukuza na kusaidia uwekezaji na; Kushauri juu ya jinsi ya kuongeza ufanisi wa uwekezaji katika uchumi
Utafiti juu ya madhara ya kufuta misamaha ya uwekezaji, huu ulilenga kutoa picha halisi ya jinsi kuondoa vivutio vya uwekezaji kunavyoathiri juhudi za kujenga uchumi kupitia uwekezaji na hivyo kuongeza madhara ya muda mrefu ya kutokuwa kwa vyanzo vya kodi.
Pia kituo kimekuwa kikifanya kazi na UNIDO katika kuandaa ripoti ya “Africa Investor Survey” na pia kuandaa ripoti ya “Tanzania investor Survey” inayotarajia kuzindulia siku za karibuni; kwa kushirikiana na UNCTAD na Benki ya Dunia kituo kimekuwa kikitoa michango mbalimbali ili kuwezesha kuandaliwa kwa ripoti nyingi za uwekezaji na kisera hasa katika sekta za kipaumbele
Maboresho na Utengenezaji wa Sera – kituo kimeendelea kuwa katika kikosi kazi cha kuboresha Sera ya uwekezaji na pia uandaaji wa Sera ya Sekta Binafsi ikishirikiana na wadau wa sekta binafsi na umma. Kazi hii imekuwa ikiratibiwa chini ya ofisi ya waziri Mkuu.
Uzinduzi wa Tovuti Mpya - Kituo cha Uwekezaji (TIC) kimezindua tovuti mpya www.tic.co.tz ambayo inatoa taarifa zote za muhimu kwa wawekezaji na wafanyabiashara. Na imekuwa ni tovuti ya kwanza kwa ukanda wa SADC kuwa na tovuti yenye maelezo ya kina kwa wawekezaji na wafanyabishara. Kanuni zipatazo 40 na taratibu 136 zimeainishwa kwenye tovuti hiyo na “link” ya tovuti ya TIC ipo katika mchakato wa kuonekana katika tovuti zote za balozi zetu za Tanzania.
Tovuti hiyo ina fomu 138 zinazosaidia maswala yote ya uanzwishwa wa biashara na uwekezaji, zikiambatana na sheria 38, ambapo zote kwa ujumla zinatoa muongozo rahisi wa jinsi ya kuwasilina na ofisi za umma zipatazo 20 na maafisa husika 88 wameainishwa kwa sura, simu zao na barua pepe kwa kumrahisishia mfanyabiashara / mwekezaji. Tovuti hii mpya inasomeka kwa lugha 80.
Muongozo mpya wa Wawekezaji “Investors Guide” inayoonyesha taarifa za uwekezaji zimegaiwa ndani na nje ya Tanzania na miongozo hiyo itaendelea kusambazwa kutokana na maombi maalum kutoka kwa wadau (physical copy) kwa uharaka “soft copy” ya muongozo unapatikana katika tovuti pia.
Tangu kuboreshwa kwa Taarifa katika tovuti Julai 2012 hadi Februari 2015 tovuti imetembelewa kwa mara 113,683 na watu kutoka katika nchi 210 duniani. Watu walioongoza kutembelea tovuti wanatoka katika nchi za Tanzania (51,519) ikifuatiwa na Marekani (6,864), India (6,408), na Uingereza (4,768). Kwa upande wa nchi Afrika inaongozwa na Kenya (3,058) na Afrika ni Afrika ya Kusini (2,640)
Mpango wa kusajili biashara na kujiunga na vivutio vya uwekezaji kwa njia ya Mtandao (Tanzania Investment Window)
Ushirikiano na taasisi za serikali kituo kimeweza kutengeneza programu ya pamoja kusajili miradi kwa njia ya mtandao ujulikanao kama TIW. Progamu hii ni endelevu na system ya kuhakikisha mwekezaji anaweza kusajili biashara, kupata Namba ya mlipa kodi na kujiunga moja kwa moja na mifuko ya hifathi jamii nchini imewezesha kupitia mtandao na mwekezaji hatatakiwa kusumbuka hata kama yupo mbali na Dar es salaam anaweza kuingia katika tovuti ya kituo na kupata maelezo na kujaza fomu moja na kuambatanisha nyaraka muhimu zinazotakiwa na kulipa kwa njia ya mtandao kwa kiwango kitakachokuwa kimeainishwa katika mtandao kutokana na aina ya huduma anayoitaka ( mobile payment au online benking) na kupangiwa siku ya kuja kuchukua cheti chake. Bado program hii haijazinduliwa rasmi ili kumalizia taratibu muhimu za taasisi zinazoshiriki. Mbeleni kituo cha uwekezaji kinaenedela na mchakato wa kumalizia vibali vingine vinavyotolewa hapa TIC viweze kupatikana pia kwa njia ya mtandao katika kujisali na hii itasaidia sana katika kupunguza urasimu katika ufanyaji biashara hapa Tanzania. Awamu ya kwanza ya program hii imefanyika chini ya ushirikiano baina ya serikali na UNDP na UNCTAD, awamu ya pili inatarajia kuanza Machi 2015 kwa ufadhili kutoka Investment Climate Facility (ICF)
Hitimisho.
Pamoja na yote haya huyu mama aliyoyafanya, yamemkuta ya kumkuta, wakati sisi tunanyanyapaa kwa mshahara wa milioni 5, sasa subirini wenzetu watakavyo mgombania!, japo hakutendewa vema, lakini you never know, everything happens for a reason, na kuna majanga mengine huwa ni blesing in disguise!.
Nampongeza kwa kazi nzuri TIC, Mungu ambariki.
Imeandikwa na Paskali.
Acha longo longo elezea mafanikio yake personally as compared to watangulizi wake otherwise sijaona ulichoandika hapo...... Hicho ulichocopy na kupest kipo kwenye website ya tic so tunajua. Mtoto aliyepatikana kwa njia haramu ni haramu tu
ReplyDeleteBwana wee lipo jambo.zaidi ya hicho ulichoandika hv kuna watu wanajua kila kitu dunia hii khaa...Raisi anajua anachofanya hafanyi tu ilimradi basi waatu wanakurupuka huko...na kuandika vitu utadhani wanajua kila.kitu...uteuzi wake umetenguliwa ipo sababu...muacheni muheshimiwa Raisi afanye kazi yake...Rungu la Jpm likikushikia limekushikia tu no mercy this tym.so tulieni wekeni vichwa maji mnyolewe...
ReplyDeleteWahanga kama Juliet ambao wameifanyia nchi hii mengi mazuri lakini leo wanaitwa "majipu" wako wengi tu.
ReplyDeleteMwingine ni yule mama wa Wakala wa Vipimo aliyesimamishwa kazi kwa mbwembwe kwa kosa la mamlaka ya bandari.
Mwandishi umeandika vizuri sana kuhusu Juliet alichokifanya TIC kwa miaka mitatu tu.
Ukipata muda nenda Wakala wa Vipimo uelezwe makubwa aliyoyafanya yule mama na akaishia kutumbuliwa bila hata huruma.
Ninachoamini ni kuwa, pamoja na nia njema sana ya Mhe. Rais JPM, by the time anamaliza miaka mitano madarakani, atajikuta anajutia maamuzi yake kuhusu baadhi ya hao wanaoitwa majipu hivi sasa.
Aidha, baadhi yetu tunafarijika kuwa pamoja na yote hayo ya dhuluma za kibinadamu, bado tunamtegemea muumba wetu kwa yote na hivyo atawanusuru "majipu" yote yaliyofanyiwa dhuluma under JPM.
Wewe unaemlaumu magufuli kwa kuwatumbua wazembe,mafisadi,wavivu,au wale wasionyesha uwezo wa kutosha kuendana na kasi ya maendeleo ya haraka Tanzania chini ya uongozi wa Magufuli inabidi ujitasmini kabla ya kutoa maoni yako. Kwa mfano nilibahatika kufanya kazi na kampuni ya kigeni hapo hapo nyumbani na mara tu waliamua kumleta meneja mpya kutoka nje na mara tu baada ya meneja mpya kuanza kazi akasema idara nyingi katika kampuni zina idadi ya wafanyakazi kuliko mahitaji ya kazi na kumshutumu meneja aliemwachia mikoba alikuwa mzembe na kuisababishia kampuni hasara kwa kuajiri wafanyakazi kutolingana na mahitaji ya kazi lakini wakati meneja wa zamani anaondoka zake kampuni ilimpatia nishani ya juu ya utendaji wa kazi. Meneja mpya akatoa sera zake,akasema sehemu ya kazi yenye idadi ya watu arobaini 40 anataka wapunguzwe hadi kufikia wafanyakazi ishini 20 tu. Watu wakawa wanajiuliza yakuwa yule mzungu alikuwa muendawazimu kwa kuwa hicho kitu hakiwezekani lakini baada ya miezi tatu kila mtu alishangaa kutokana na mabadiliko makubwa ya maendeleo yalioletwa na meneja mpya. Sera zake zilikuwa simple ni ufanisi bora kutokana na wafanyakazi wachache wanaojitambua wanaotunzwa vizuri kutokana na mahitaji ya kazi na sio blah blah. Maghufuli hana blah blah ni mtu wa kazi,watanzania blah blah na kujifanya tuna uweledi juu ya kila kitu ni kilema tunachojisifia nacho kuwa ni kitu kizuri. Kwa kweli inabidi tumtasmini sana Magufuli kama kweli ni mtanzania? Kutokana na utendaji wake wa kazi iliotukuka. Na kama kweli ni mtanzania halisi basi atakuwa ni mtanzania wa ajabu sana kwani mtanzania kama si fisadi atakuwa mwanisiasa muongo. Na kama atakuwa si mwanasiasa muongo atakuwa tapeli,na kama si tapeli basi ni mzembe ilimradi ni sifa zetu watanzania yakaribu asilimia 80%, kwa hivyo tumuache Magufuli afanye kazi yake kwa manufaa ya Tanzania na watanzania sio kwa maslahi ya mtu binafsi.
ReplyDeleteSo boring.unaweka gazeti.
ReplyDeleteMwache Juliet aseme mwenyewe, tunakua kama mashabiki wa simba na yanga, mpira unchezwa uwanjani, lakini mashabiki wanazimia jukwaani na kutoana ngeu mtaani.
ReplyDeleteSiamini kuwa raisi anafanya kazi kwa kusikiliza majungu na kama anafanya hivyo basi hafai,ila ninachojua kwa uelewa wangu mdogo ni kwamba anatekeleza kwa kupitia vyombo vyake vya ujasusi, labda niambiwe kuwa hivyo baadhi vina mabifu na wanaotumbuliwa na wamempata kiongozi asiyefuata kanuni na sheria za nchi. Watanzania tufike mahali tuwe wazalendo tusishabkie tu jambo kisa mhusika anakugusa kwa namna fulani yoyote ile. Nchi hii haikupaswa wananchi wake wakose kupata huduma kutoka serikali yao kwa raslimali ilizonazo ni nyingi mno. Kabla ya mwaka 1980 tulikuwa tukipata huduma zote bure na mtoa huduma hakudhubutu hata chembe kuomba chochote iwe kwa maneno au ishara , na wakati huo nchi ilitegemea sana kwenye kilimo ,iweje leo serikali ishindwe kutoa huduma hizo na huku vyanzo vya mapato vikiwa vimeongezeka mno? hata kama idadi ya watu imeongezeka lakini kwa ratio ileile .
ReplyDelete