Mange Amshukia RAY C Sakata la Matumizi ya Madawa ya Kulevya..Atoboa Siri ya Ray C Kuondolewa Kwenye Progarm ya Methadone

Katika Jitihada za kumsaidia Ray C , Mange Kimambi Amefunguka Haya Hapa Chini:

"Confirmed news, Ray C ametolewa kwenye program ya kunywa dawa ya Methadone Mwananyamala Hospital. Alikuwa kila akipimwa mkojo anakutwa bado anatumia. Pale wanatoa dawa kwa masharti.Ray C anaweza kukaa wiki hajaenda kunywa dawa, ile dawa hakuna mgonjwa anaweza kukaa siku hata 1 hajanywa, Arosto yake ni hatareeeeee unaambiwa bora Arosto ya heroine kuliko Arosto ya methodone, so ukiona mgonjwa kapitisha hata siku moja hajafika kunywa dawa ujue tu anatumia Tena hata bila kumpima mkojo. Sasa Ray C alikuwa anakata wiki hajafika kwenye dawa . Ndo wakaona wamkatie mbali. Ambao bado mnamtetea Ray as if nyie ndo mnampenda sana nenda pale wanapopokea dawa kila siku Kama utamuona Ray C. Huyo boyfriend wake wa Sasa anaitwa Frank alikuwa rafiki wa Lord Eyes,ni muuzaji na mtumiaji, Kwahiyo hapo ni parefuuuu....

Anyways point sio kumwanika Au kumwandama huwa nawapinga mno global Kwa kuandika habari za uongo Kila siku Ila Kwa hili la kumwandama Ray C acha wamwandame wanamsaidia . Maana Ray C anafanya juu chini kuaminisha watu uongo ili aendelee kujimaliza.

hata Mimi sijui anasaidiwaje , Kama rehab keshapelekwa, Kama methadone keshakunywa sijui kilichobaki. Tusichukulie hii issue kijuu juu huyu msichana akiachwa Sasa hivi atawajoin kina Whitney Houston kiutani utani Hivi Hivi.... Embu tushauriane jinsi ya kumsaidia Maana Mimi sina idea aiseeee.... Alafu akifa tutajisikia vibaya mnoooo kuwa tulikaa pembeni tunaangalia. Sitaki kujua mama yake ana hali gani 🏽. Watoto wanajua kutesa wazazi jamani, I can't imagine mtoto wangu mmoja aje kuwa hivi jamani naweza kufa kwa kuumwa roho !

Challenge kubwa ya kuwasaidia addicts inabidi wawe tayari kubadilika. Inabidi wao wenyewe ndo waamue na sio mtu umforce. Yani Ray C inabidi aamue she wants to live" 

Source:Mangekimambi Insta

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wazo: Baba yake Kikwete amtembelee labda atamwonea aibu.

    ReplyDelete
  2. Jamni jamn jamn jamn yani naishiwa maneno nasihiwa pumzi eeh Mungu ingilia kati kizazi kinateketea...Mungu naomba unilindie watoto wangu wewe ndo unaweza kuwakuza vyema mm siwezi daah jamn ray c y jamn y mamy unarudi kulekule...asaidiwe jamn wadau wa muziki msaidieni ray c..wauza madawa ya kulevya mlaaniwe nasema mlaaniwe nyie na vizazi vyenu

    ReplyDelete
  3. Inabidi afungiwe ndani hasitoke nje

    ReplyDelete
  4. Mbona hii picha ya zamani

    ReplyDelete
  5. muacheni afe si mtu mzima ana akili zake ndio maisha aliochagua akili zake zilimtuma hivo afe tu hana faida

    ReplyDelete
  6. MUNGU MFUNGUE PLEASE

    ReplyDelete
  7. madawa ya kulevya si vitu vya kuchezea hivi vijana mnaotumia madawa mnafikiri madawa yatawasaidia kutatua matatizo yenu au yatawasaidia kupunguza stress? Jibu ni big No, wadawa yanawaongezea matatizo vile vile yanaharibu ubongo pamoja na afya ya binadamu, vile vile yanawaharibia maendeleo yenu mnakuwa hamfiki popote, vile vile mara nyingi husababisha vifo vingi, kwani ni wasanii wangapi wamekufa na madawa pia na wale wasiokuwa wasanii ambao ni watu wa kawaida. Yaani nyie vijana mnaotumia madawa hamna huruma kwa ndugu zenu,marafiki zenu na watu ambao wanaowapenda? Kwani hamna njia nyingine ya kutumia kupunguza mawazo ambayo ina nafuu, ni heri hata mtu unywe bia kama walio wengi wanywaji sio wajinga wamechagua njia nafuu na yenye uhalali, mimi mwenyewe nimekulia maisha ya tabu utotoni kuachwa na wazazi wangu ambao walihamia bara lingine majuu na kuniacha bila hata kuniaga leo nimekuwa mtu mzima pia najitegemea mwenyewe lakini siwezi samehe wazazi wangu hadi leo nikifikiria maisha yangu ya utotoni huwa inaniuma sana lakini hata siku moja sijawahi kufikiria kutumia madawa, sababu nikiwa na matatizo naongea na saikolojia na ndiyo imenisaidia sana lakini sio kilevi.

    ReplyDelete
  8. Oneni Langa Kileo masikini amejiondokea akiwa bado kijana lakini bado tu hamjifunzi na masikini Langa alikuwa akiimba kujitabiria kifo chake sababu alikuwa anajua madaya yanaweza kumuua

    ReplyDelete
  9. bora upige punyeto uondoe stress lkn sio kula poda

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad