Vyama vya siasa na wadau mbali mbali wameendelea kupinga hatua ya bunge la jamhuri ya Muungano kuzuia vyombo vya habari kurusha mijadala ya bunge kwa njia ya television na radio mpaka pale habari hizo zitakaporekodiwa na kitengo cha habari cha bunge na kusambazwa ktika vyombo vya habari ili zirushwe.
M/kiti wa chama cha kijamii cha CCK Renatus Muhabi akizungumza na waandishi jijini dsm amesema hatua ya bunge kuzuia waandishi wa habari kupata habari au kurusha moja kwa moja inarudisha nyuma maendeleo,kuwanyima wananchi kupata habari kwa waliowachagua lakini pia ni ukiukwaji mkubwa wa demokrasi ya habari nchini.
Katika hatua nyingine chama hicho leo kimewapokewa Viongozi waandamizi kutoka chama cha UDP ambao wameamua kujiunga na CCK kwa ajili ya kuendesha harakati za kisiasa nchini.
Wakizungumza mara baada ya kukabidhiwa kadi na M/kiti wa Cck wamesema wamehama UDP kwa madai kuwa chama hicho kimeshindwa kuleta mabadiliko ya kweli .