Michezo ya viporo ya Ligi Kuu soka Tanzania bara imepigwa leo kwa vilabu vya Azam FC na Yanga kucheza michezo yao ambayo awali ilikuwa imehairishwa kutokana na kuingiliana na michezo yao ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, lakini na michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa upande wa Yanga.
Yanga walikuwa uwanja wa Taifa Dar Es Salaam kucheza dhidi ya Kagera Sugar ambao awali walianza kucheza kwa kasi na kufanikiwa kupachika goli la uongozi dakika ya 9 kupitia kwa Mbaraka Yusuph, dakika 16 baadae Donald Ngoma akaisawazishia Yanga na kwenda mapumziko kwa sare ya 1-1.
Wakati Kagera Sugar wakitafakari namna ya kupambana kipindi cha pili na kuifunga Yanga, Amissi Tambwe aliongeza goli la pili dakika ya 18 baada kipindi cha pili kuanza na Haji Mwinyi akahitimisha ushindi wa Yanga wa 3-1 dakika ya 88 kwa kufunga goli la tatu.