Meneja wa Q Chief na MB Dog Afunguka...Nimeshatumia zaidi ya Bilioni Moja Kuwasaidia Wasanii

Mkurugenzi wa label ya ‘QS Mhonda Entertainment’ QS Mhonda amesema toka aanze harakati za kusimamia muziki tayari ameshatumia zaidi ya bilioni 1.
234

Mfanyabiashara huyo wa majengo ambaye label yake ya ‘QS Mhonda Entertainment’ inamsimamia, MB Dog, Q Chief, Mzee Yussuf pamoja bendi ya QS International Band, ameiambia Bongo5 Jumatano hii kuwa hela hizo amekuwa akizitumia katika nyakati tofauti tofauti.

“Kusema kweli bado sijarudisha pesa yangu na tayari nimeshatumia zaidi ya bilioni 1 kwenye muziki, yaani ni kama nawasaidia tu,” alisema QS Mhonda. “Kwa hiyo hii ni sehemu ya maisha yangu kwa sababu wakati natafuta hela nilimuomba mungu anipe pesa ili na mimi niweze kuwasaidia watu kama hawa, ndicho nachokifanya sasa hivi,”

Aliongeza,“Mimi nimemsimamia Nay wa Mitego, nikamnunulia gari mpya, H. Baba amepita kwangu. Pia niliwai kumleta hapa nchini JB Mpiana, project ambayo iligharimu zaidi milioni 300. Pia kuna hawa wengine kama akina Mzee Yussuf ambao huwa nawasaidia mara moja moja, kwa hiyo kusema kweli ni gharama kubwa sana,”

Chanzo: Bongo5
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad