Mirror Chini ya Management ya Wema Sepetu Umewaangusha Mashabiki Wako, Utawalipa Nini?

Marehemu Albert Mangwair alikuwa mtu wa mwanzo kutambua kipaji cha muziki alichokuwa nacho Mirror pamoja na Jordan.

Kwa mara ya kwanza watu walimtambua kwenye nyimbo yake ‘One and Only.’ Kiukweli huu ni wimbo mzuri ambao unaweza kuwarudisha karibu watu waliotengana kwenye mahusiano pindi watakapousikiliza wimbo huo.

Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi, shukrani za dhati zimuendee Wema Sepetu aka Madam Sepetunga, aliyefanikiwa kumchukua Mirror na kuanza kusimamia kazi zake za muziki chini ya kampuni yake ya ‘The Endless Fame’.

Miaka inazidi kwenda lakini bado hatujamuona yule Mirror ambaye tulimtarajia atakuja kuwa ni miongoni kati ya wasanii watakao hit ndani hadi nje ya Tanzania.
Ni takribani miaka mitatu mpaka sasa tangu Mirror awe chini ya menejimenti hiyo na tayari ameshafanikiwa kuachia nyimbo kadhaa kama, ‘Hapo Ulipo’ na ‘Naogopa’.

Japo ameweza kuwa chini ya menejimenti yenye uwezo mkubwa wa kupata support na uwezekano wa kufanya vizuri lakini hali imekuwa ngumu kwa Mirror na kila siku anapoachia wimbo anazidi kuonekana ni kama msanii anayechipukia.

Nahisi inaweza ikawa kama hadithi ya sungura na kobe. Angalia alipotoka Baraka Da Prince mpaka leo amekukuta hapo hapo ulipo umelala usingizi mzito na amezidi kukuacha.

Sitaki kuamini kama ni kweli umeridhika na mafanikio ya huu muziki, hebu angalia wasanii wengine waliopata mafanikio zaidi lakini bado wanaendelea kupambana zaidi.

Ukiangalia mwanzo wakati anaanza, alifanikiwa kupata mashabiki wengi ambao walitarajia kuwa atakuja kufanya makubwa lakini kumbe’ Umdhaniaye ndiye kumbe siye’.

Muda bado upo bado hujachelewa, amka kwenye usingizi mzito uliolala acha kuridhika kwenye ndoto wakati hujapaona ulipotakiwa kufika
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad