Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda Apiga Marufuku Kilevi Aina ya Kiroba

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda amepiga marufuku uuzwaji wa kilevi aina ya kiroba katika mkoa huo.

Alisema uamuzi huo unatokana na vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa kushindwa kufanya kazi na kulewa wakati wa kazi.

Aidha mkuu huyo wa mkoa alisema anafanyia kazi sakata la mkazi wa Kata ya Ngarenaro anayedaiwa kujihusisha na uuzaji na uingizaji wa dawa za kulevya ambaye baada ya kukamatwa na polisi aliachiwa katika mazingira ya kutatanisha.

Ntibenda alisema hayo jana Arusha wakati akizungumza na watendaji wa serikali za mitaa 154, maofisa watendaji kata 25 pamoja na wenyeviti wa serikali za mitaa.

Alisema suala la kilevi aina ya kiroba ni kero kwa vijana kufanya kazi wakiwa wamelewa au kuwa navyo mifukoni hasa madereva wa pikipiki, daladala na wapiga debe.

Alisema kutokana na vijana kunywa kinywaji hicho nyakati za kazi, amepiga marufuku uuzwaji wa kilevi hicho, atakayekiuka agizo hilo hatua za kisheria zitachukuliwa.

“Sitaki kuona viroba vikiuzwa katika Mkoa wa Arusha na atakayekiuka nitamchukulia hatua za kisheria, lakini huyu anayeuza dawa za kulevya halafu polisi wanamwachia na wananchi hawajui kwanini anaachiwa huku akiendelea kuuza dawa, sasa nasema mwisho wake umefika, nitafuatilia kwa makini suala hili.”

Baadhi ya wenyeviti wa serikali za mitaa walihoji sababu za kutokuwa na ofisi za kufanyia kazi badala yake wanalazimika kutumia nyumba zao au kukodisha ofisi ili kufanya kazi za jamii lakini pia hawana posho za vikao.

Wenyeviti hao akiwemo Amani Mwakalinga wa mtaa wa Darajani na Hilary Mkonyi wa mtaa wa Ngarenaro, walisema awali Mkurugenzi wa Jiji, Juma Idd aliahidi kuwajengea ofisi lakini hadi sasa hakuna utekelezaji.

DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL BLOG HAPA
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. viongozi wetu wanapenda kukurupuka hawajui viroba vinasaidia pato la taifa kwenye kodi

    ReplyDelete
  2. Ukisikia kukurupuka ndiko huku.Statistics zinaonyesha kuwa asilimia 85% ya wanywaji wa pombe nchini hunywa pombe za kienyeji,11% hunywa bia,4% hutumia pombe kali na 1% wine.
    Sasa huyu mkuu anatumia takwimu zipi kuhusisha viroba na ongezeko la ulevi? Badili ya kupambana na wapiga gongo u naondoka kilevi kilichotengenezwa kitaalamu,kinachoongeza path la taifa kupitia kodi.

    ReplyDelete
  3. Hii ndio ndoto ya Tanzania inayojenga uchumi wa viwanda.kupiga hatua mmoja mbele kisha 2 nyuma.

    ReplyDelete
  4. walevi acheni kutetea ulevi, mkuu wa mkoa toa hivyo viroba wakinywa wanakuwa na macho mekundu na wanatoa harufu mbaya kinywani.!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hujui unaloongea,mshahara wako unatoka kwenye viroba hivyox2.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad