Msanii wa Muziki wa dansi Ndanda Kosovo Afariki Dunia

Msanii wa muziki dansi, Ndanda Kosovo amefariki dunia Jumamosi hii katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akitibiwa maradhi ya tumbo.
ndandaaa

Taarifa za awali zinasema marehemu alifikishwa hospitalini hapo kupata matibabu ya vidonda vya tumbo vilivyokuwa vikimsumbua siku chache zilizopita lakini alifariki mapema asubuhi ya leo.

Mmoja wa viongozi wa wanamuziki wa Kongo chini Tanzania, King Dodoo amethibitisha kutokea kwa msiba huo na kusema kuwa Ndanda Kosovo alifikishwa Hospitali ya Mwananyamala juzi na kulazwa tatizo la maradhi ya tumbo.

Baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya, jana alihamishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako mauti yamemkuta leo asubuhi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad