Mtoto wa Miaka Miwili Amuua Mama yake Kwa Risasi

Mtoto mwenye umri wa miaka miwili amemuua mama yake mzazi kwa bahati mbaya katika jiji la Milwaukee nchini Marekani, baada ya kuikuta bastola nyuma ya gari walilokuwamo.

Mwanamke huyo kwa jina la Patrice Price alikuwa akiendesha gari la mpenzi wake ambaye anafanya kazi za kiusalama nchini humo.

Polisi wa Milwaukee wamesema kuwa mwanamke huyo alipigwa risasi moja mgongoni ndani ya gari hilo ambalo pia kulikuwa na mama wa Prince ambaye ni bibi wa mtoto huyo pamoja na mtoto mwingine wa mama mwenye umri wa mwaka mmoja.

Mwezi mmoja uliopita mtoto mwenye umri wa miaka minne huko Florida alimpiga risasi mama yake mzazi aliyejulikana kwa jina la Jamie Gilt katika tukio linalofanana na hilo japo mama huyo hakupoteza maisha.

Pichani ni marehemu Patrice Price
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HAYO YOTE SABABU YA BASTORA ZA BANDIA. VITU VINGINE HAVIFAI KUWA NA VYA BANDIA VYAKE!!!

    ReplyDelete
  2. anonymous APRIL,28 ,kwa nini unafikiri ni bandia?hapo kinachoonekana ni uzembe ti wa kuhifadhi situ vya hatari...ndo maana watu walio makini huwa wanaonya..WEKA MBALI NA WATOTO..

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad