Mtu Aliyeambukiza Ukimwi Watu 200 Afungwa Miaka 25 Jela....

Daktari aliyewaambukiza wagonjwa 200 virusi vya ukimwi nchini Cambodia amehukumiwa jela.Daktari huyo bandia alipatikana na hatia ya kuwaambukiza takriban watu 200 virusi vya ugonjwa wa Ukimwi amehukumiwa kifungo cha miaka 25 jela kwa makosa yake.

Baadhi ya wahasiriwa wa makosa hayo wamekwisha fariki dunia, Yem Chrin alikuwa akitumia sindano zilizokuwa zimekwisha tumika kuwatibu wenyeji wa kijiji cha Roka bila ya kujua alickuwa akisambaza Virusi vya Ukimwi.Awali Chrin alikuwa ameshtakiwa kwa mauaji lakini upande wa mashtaka ukabadilisha shtaka na kuwa kuua bila ya kukusudia.

Kesi hiyo imefichua uhaba wa madaktari na ugumu ulioko kwa raia kupata huduma za afya katika maeneo mengi ya vijijini nchini Cambodia.

Utafiti umebaini kuwa zahanati nyingi katika maeneo ya vijijini huendeshwa na madakatari bandia ambao hawajahitimu kuwatibu wagonjwa.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mimi nilifikiri huyo daktari alikuwa na ukimwi halafu akaambukiza watu, kumbe kichwa cha habari kinasema tofauti na histori yake, kumbe daktari alikuwa hajafanya makusudi kuwaambukiza watu bali ni uhaba wa madaktari pia alikuwa hana ujuzi na hapo pia liko kosa kwa huyo aliyemwajiri mtu asiye kuwa na elimu au ujuzi wa udaktari, hayo mambo ya kuambukizwa hospitari yalikuwa pia yanatokea Tanzania enzi za miaka 1980 mpaka miaka ya 1990, lakini sasa ni 2016 lazima watu wangekwisha kujua kuwa kuna gonjwa baya la ukimwi na kujua na kutozembea kuwaajili watu haswa kwenye hospitali ambao hawana vibari vya kufanya kazi mahospitalini hata kama ni nchi maskini au vijijini huo na kama mtu huna kibali cha kufanya kazi hospitali kwa nini ukubali kufanya kazi hospitalini na kuhatarisha maisha ya watu ona sasa huyo jamaa keshaua watu na kuwaambukiza wengine wengi. Na anastahiri kwenda jela

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad