Usiku wa April 24 imetangazwa good news kwa soka la Afrika, huu sio ushindi wa taifa la mchezaji husika ila ni fahari ya Afrika nzima, winga mshambuliaji wa kimataifa wa Algeria anayeichezea klabu ya Leicester City ya Uingereza Riyad Mahrez ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya PFA 2015/2016 (Professional Footballers Association).
Riyad Mahrez ametangazwa kushinda tuzo hiyo mbele ya wachezaji kama Mesut Ozil wa Arsenal, Jamie Vardy wa Leicester City, Harry Kane wa Spurs, N’golo Kante wa Leicester City, Dimitri Payet wa West Ham United, PFA ni tuzo za wachezaji bora wa kulipwa.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Riyad Mahrez ndio alikuwa mchezaji wa Algeria aliyefunga goli la nne dakika ya 43 katika ushindi wa goli 7-0 dhidi ya Taifa Stars November 17 2015 na kuIondoa Tanzania katika mbio za kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2018.