Mwanamke aliyeolewa ni msaidizi wa mume wake, kuhakikisha amempikia mumewe,amemfulia, na mumewe akitoka kazini akili zake zote ziwe kwake, amuhudumie kwa kila kitu akisimama katika nafasi yake kama mwanamke aliyeolewa. Pia mwanamke aliyeolewa ni nguzo ya familia yampasa kuwa mtu anayemwomba Mungu kwa Imani yake kila wakati na pia kuwalea watoto vizuri na kuhakikisha usalama wao,
Siku hizi smartphone zinatuponzaa wanawake, kila saa tuko mitandaoni, mara kutafuta umbea, mara kuupload picha zisizo na mantiki et umepita kwa mangi umenunua kachips umepiga picha chaap umepost, mara kuandika status za vijembe watsapp, mara kutukana kwenye mitandao,
mwanamke umeolewa una account 20 insta,magroup yasiyo na maana ndo usiseme, mume karudi kazini wewe huna habari umetundika miguu uko busy na simu housegirl ndo amuhudumie mumeo chakula, we unafanya kuagiza tu nipe hichi mnawishe baba mikono kweli jamani?, smtms hadi unapika chakula kinaungua kisa ukobusy na simu.
Mara umepigiwa simu na mwanaume gani sijui anaongea upuuzi wewe ni kuchekacheka tu .Shost anakupigia simu nusu saa mnaongea tu upuuzi,hadi mwanaume anaboreka akikusubiria umalize kuongea aseme nawe jambo.
watoto wala huna habari nao hujui kwamba wamekula,hujui yupi ana homa, ni housegirl ndo anakuja kukuambia mama, Debora joto lake leo liko juu.mama mtu hujui kama joto la mtoto liko juu ila unajua picha ya mwisho leo wema sepetu kaweka insta kweli???? Halafu unajiita umeolewa wakati hujui majukumu yako kama mke??.
Aisee Wanawake mlioolewa badilikeni, simaanishi kwamba msitumie smartphone ila muwe na kiasi, hii ya mke wa mtu kiiila saa uko mitandaoni pasipo na sababu ya msingi acheni,waachieni single Girls.