Naibu Spika Dk. Tulia Akson Atumia Mil 20/- Kumshukuru Mungu


Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Akson ametoa Sh. milioni 20 na zawadi mbalimbali kwa jamii wilayani Rungwe mkoani Mbeya, ikiwemo shule ya walemavu wa mtindio wa ubongo na albino kama shukrani kwa Mungu.

Kitendo hicho cha kutoa zawadi ya zaidi ya Sh. milioni 20 kilipongezwa jana na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Zainab Mbusi, ambaye alisema amefarajika kuona mbunge huyo amefika wilayani humo na kusaidia shughuli za kijamii hasa katika shule, Kanisa na vikundi vya wajasilia mali.

Alisema katika Shule ya Msingi Mabonde alikosoma, Dk. Tulia alitoa Sh. milioni 5 kwa ajili ya ukarabati wa majengo na katika Shule ya Sekondari ya Loleza ya wasichana Mbeya alikosoma pia, alitoa Sh. milioni 5.

Mkuu wa Wilaya huyo alisema Naibu Spika alisaidia pia walemavu wa mtindio wa ubongo na albino Sh. milioni mbili kwa ajili ya ujenzi wa uzio kwenye jengo lao.

Mbusi alisema amepewa kazi ya kuhakikisha anasimamia fedha hizo ili zitumike kama zilivyokusudiwa na kuwataka wadau wengine kuiga mfano wa Dk. Tulia kwa kukumbuka kwao na kusaidia shughuli hizo na kupunguza changamoto zilizopo.

Katika hatua nyingine, DC huyo aliahidi kuitisha harambee kwa wadau kwa ajili ya kutafuta fedha zitakazotumika kununua madawati ili kupunguza upungufu wa madawati wilayani humo ambapo katika halmashauri ya Rungwe pekee yanahitajika 8,000.

Alisema katika kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa, ametafuta wadau ambapo Shirika la Kimarekani la Africa Bridge limetoa madawati 2,000 huku wadau wengine akiwemo mfanyabiashara anayemiliki mabasi, Yona Sonelo wameahidi kuchangia.

Aliwataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha zoezi hilo linakamilika ili kuondoa tatizo la madawati linalopelekea wanafunzi kukaa chini na kuwa nyuma kulinganisha na wilaya za mikoa ya kaskazini ambazo zimepiga hatua katika sekata ya elimu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad