Nashusha Balaa Lingine Muda si Mrefu- Ali Kiba

Msanii Ali Kiba ambaye kwa sasa anafanya poa na kazi yake ya Lupela amefunguka na kusema kuwa muda si mrefu kutoka sasa ataachia kazi nyingine mpya.

Msanii Ali Kiba akiwa studio za East Africa Radio kwenye kipindi cha Planet Bongo.
Akipiga stori kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Ali Kiba amedai kuwa kazi yake hiyo anayotaka kuiachia mpaka sasa hana jina lake lakini atawaachia mashabiki ambao ndiyo watakuwa na jina la kazi hiyo.

"Mashabiki zangu kaeni mkao wa kula nashusha balaa lingine muda si mrefu kutoka sasa. Hii ngoma hata sijui mimi niiiteje yaani ila nitawaachia wenyewe wananchi mchague jina la kazi hiyo" alisema Ali Kiba.

Mbali na hilo Ali Kiba amesema kuwa kitendo chake cha kutoa wimbo bila video kimekuwa na athari kubwa kwake kwani wimbo unakuwa mkubwa na mashabiki wanakuwa tayari na video zao vichwani mwao, kiasi kwamba anapokuja kutoa video ya wimbo huo unakuwa tofauti na mategemeo na matarajio ya baadhi ya watu jambo ambalo huwa linaleta maneno maneno.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nakupigia salute Single boy
    shabiki wako kutoka Oman

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad