Ni Kweli Kanye West Alilazimishwa Kupiga Picha na Diamond?

Ni takribani mwezi mmoja sasa tangu Diamond na Kanye West walipokutana kwenye uwanja wa ndege, Los Angeles nchini Marekani na kupiga picha ya pamoja.


Hivi karibuni maneno yameanza kuzuka tena mitaani kuhusu picha hiyo waliyopiga Diamond na Yeezy. Watu wanazungumza kwanini alinuna kwenye ile picha?

Akiongea kwenye stori tatu ya Planet Bongo, inayoruka kupitia EA Radio, Diamond amesema, “Nafikiria ni attitude ya Kanye ndivyo alivyo.”

“Ananuna hata akipiga picha na mkewe na mkwe wake, nafikiria nilipata bahati kwenye ile picha yangu kidogo alifurahi. Kuhusu collabo chochote kinaweza kutokea tumuombe Mungu. Naposema nataka muziki wetu upenye Marekani ni kujaribu kwenda kupambana na wale manguli wao ili tuone itakuwaje,” aliongeza.


Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. huyu bwege anafikiri kupiga picha na hawa jamaa ni dili!! kwanza hapo Kanye kasmile wapi? yani yeye mwenyewe anajitamba kama mwanamuziki mkubwa lakn bado anadandia kupiga picha na wengine! hovyoooo!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Basi mwanamuziki mkubwa ni wewe na ukoo wako,kapigeni picha na Kiba sasa!

      Delete
  2. Nyie wote mnaomtusi Dimondi hamna hata haya mmeona mwenzenu kafanikiwa kimaisha mnaleta fyofyoko hamna kazi za kufanya au hamna mawazo mengine ambayo yatawafanya mjikidhi kimaisha nyooooooooooooo! mwacheni mtoto wa mwanaume/mwanamke mwenzenu

    ReplyDelete
  3. Hanithi wa kwamtogole huyoo kwani hunjui anavyopenda kiki.

    ReplyDelete
  4. masikini akipata kila mtu atajua!!!

    ReplyDelete
  5. WIVU WENU TU. DIAMOND WEE PIGA KAZI ACHA WASEME HAWANA KITU HAO. WANA WIVU HAO.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad