NSSF yazidi Kuumbuka: Ufisadi wa Ujenzi wa Hoteli Mwanza, Jengo la Biashara Mzizima


Kwa kashfa hizi, watetezi wa Dr Dau washaumbuka, maana tuliambiwa hakuna mtu wa kuziba pengo lake, kumbe siri ni upigaji deal tuuu.

=> Ujenzi wa hoteli Mwanza, kampuni mbili zapewa mabilioni kwa kazi zile zile

=> Mkandarasi wa ujenzi wa jengo la Biashara la Mzizima azidishiwa malipo.

=> Ujenzi wa hoteli ya kitalii Mwanza, wakandarasi walizidishiwa zaidi ya Bilioni 16 sawa na asilimia 23 ya mradi wote bila sababu za msingi.

=> Kuhusu ujenzi wa jengo la biashara Mzizima Tower ni kwamba kampuni tatu ziliomba mradi huo ambazo ni Atlas, Ginde na Jandu ambayo ilishinda.

Wataki wa kuwasilisha maombi ya zabuni ya Jandu ilikuwa sh. 8,346,155,654 lakini kamati ya Tathmini iliketi na kupitia upya mkataba na kubaini makosa hivyo ilirekebisha zabuni hiyo isomeke 8,340,700,710.94 pamoja na ongezeko la Thamani (VAT). Jandu aliridhia marekebisho hayo.

Pamoja na marekebisho hayo, mkataba waliosainiana kati ya NSSF na Jandu ulikuwa wa kiwango kile kile kilichokosewa cha sh. 8,346,155,654 chenye ziada ya sh. 5,454,943.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. vyombo vya habari navyo vinatumika kuchafua fua watu hasa haya magazeti

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad