Obama: Tulikosea Sana Kuivamia Libya na Kumuondoa Muammar Gaddafi


Rais wa Marekani Barack Obama amekiri kwa mara ya kwanza kwamba serikali yake ilifeli katika kutatua mzozo wa Libya.


Amesema hilo huenda ndilo “kosa kubwa” zaidi alilolitenda wakati wa utawala wake.


Bw Obama amesema Marekani haikua na mpango mahususi wa jinsi taifa hilo litakavyotawaliwa baada ya kuondolewa madarakani kwa Kanali Muammar Gaddafi.


Alisema haya katika mahojiano na runinga ya Fox News kuangazia mafanikio na mapungufu ya utawala wake.


Hata hivyo ametetea hatua ya kuingilia kijeshi nchini Libya. Marekani na Muungano wa NATO zilitekeleza mashambulio ya anga kuwalinda raia baada ya kuzuka maasi dhidi ya Muammar Gaddafi mwaka 2011.


Lakini baada ya mauaji ya kiongozi huyo, Libya ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya makundi ya waasi huku makundi mawili yakiunda serikali na mabunge tofauti.

Katika hatua za kurejesha utulivu serikali ya muungano wa kitaifa inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa imewasili katika mji mkuu Tripoli ili kuanza mipango ya kuongoza nchi ya kurejesha hali ya kawaida.


Uchaguzi mkuu nchini Marekani utafanyika Novemba na Rais Obama atakabidhi madaraka kwa mrithi wake Januari mwakani baada ya kuongoza kwa mihula miwili.


Chanzo: BBC
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hizo ndizo desturi zao kuwaondosha viongozi wasiokubaliana na mahitaji yao. Wakiona ulimwengu umewashtukia wanajidai wamefanya makosa. Sasa yupi mwengine yupo kwenye rada yao magufuli? Maana washaanza na sababu za pesa za mcc. Kazi kuvamia nchi za watu Washenzi kabisa.

    ReplyDelete
  2. Hizo ndizo desturi zao kuwaondosha viongozi wasiokubaliana na mahitaji yao. Wakiona ulimwengu umewashtukia wanajidai wamefanya makosa. Sasa yupi mwengine yupo kwenye rada yao magufuli? Maana washaanza na sababu za pesa za mcc. Kazi kuvamia nchi za watu Washenzi kabisa.

    ReplyDelete
  3. Kote walikovamia mpk leo amani hakuna ipo cku RIP Gaddafi tutakukumbuka daima

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad