Ofisi ya Waziri Mkuu Waamua Kutumia Bajaji na Piki Piki Kubana Matumizi...Mashangingi Sasa Basi


Dodoma. Kamati ya Katiba na Sheria ya Bunge imeipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kutenga fedha ya kununulia bajaji na pikipiki zitakazotumiwa na watumishi kwa mwaka huu wa fedha, ikiwa ni mkakati wa kubana matumizi.

Wizara iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ni ya Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Walemavu.

Akiwasilisha maoni ya kamati hiyo kwa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu ya mwaka 2016/17, mwenyekiti wa kamati hiyo, Mohamed Mchengerwa amesema uamuzi wa namna hiyo unaendana na dhana ya kubana matumizi ya fedha ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Hata hivyo, hotuba ya bajeti iliyosomwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo, haionyeshi pikipiki na bajaji hizo zinanuliwa kwa ajili ya wafanyakazi wa kada gani.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ndiyo hii haswa tuliota kuiona to aka awali

    ReplyDelete
  2. Mph Majaliwa okoeni hii nchi.. ufidadi na ubadhitifu muukataee kabisa..he kwa hii hatima undani ya maana mmoja that bana matumizi ya Kiasi gani??

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mimi sijaelewa, ndio umeandika nini sasa?

      Delete
  3. Wacha waisome number

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad