Paul Okoye wa kundi la P-Square Anaswa South Africa Akiwa Amevaa Kofia ya WCB Wasafi ya Diamond..

Ukimuona Paul Okoye wa kundi la P-Square akiwa amevaa kofia ya WCB na yupo Johannesburg, Afrika Kusini ambako Diamond yupo huko tangu mwanzoni mwa wiki hii kuzindua video ya Colors of Africa, ujue mambo yameiva.

Paul amepost picha Instagram akiwa amevaa kofia nyeupe ya WCB, label ya Diamond na kuashiria kuwa huenda wiki hii wakali hao wakashoot video ya collabo yao. Diamond aliingia studio na P-Square mwaka jana.

Kituo cha runinga cha MTV Base kiliripoti wiki hii kuwa Diamond atashoot video ya wimbo huo hivi karibuni.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Cha ajabu nini sasa mbona watu wana vaa jezi za lakers,chata za nike na adidas kofia za Newyork hata hawajawahi kufika si nembo tu hiyo kuvaa kofia ya wasafi nayo habari????

    ReplyDelete
  2. Keep it up Diamond! I like it.

    ReplyDelete
  3. Anonymous 8:23 acha wivu ww,hongera diamond p-squareni wasanii wakubwa hawavai lebo kizembe zembe

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad