Kwa mujibu wa taarifa nlioipata toka.kwa grup la wasapu inasema
Mdada ambae ni mpendwa aliomba ruhusa kwa mumewe anaenda kwa maombi /mkutano wa injili Mbeya jamaa akamkubalia kumbe moyoni anamsaree.. mke alipotoka kupanda daladala mume nae akapanda la kwake walipofika stand mdada akapanda gari ya kyela na mumewe nae akamfata (bila mke kujua).
Mwanamke akafika guest na mchepuko ulikua ushafika na mume bae akafikia guest hiyo hyo bila bibie kujua,sasa baadae usiku mme akaenda kugonga rum ya bibie na mchepuko bila kujua wakafungua mlango .
Mme alikua na tindikali iliomixiwa kwa "uweledi" wa hali ya juu, akawamwagia na mwishowe akajimwagia.
Hizo picha ndo matokeo ya tindikali.
Mie sielewi kabisa wivu wa sasa unapoelekea..hivi hao waume hawaoni wake wengine duniani ila hao walokwisha Mughsi Mungu?..similarly na iliyojitokeza Zenj,mume mtu kujirusha toka ghorofani na mke we, kisa! fumanizi (wivu)..how come uamue maamzi kama hayo ya kumtoa uhai mwenziwe na wewe mwenyewe hali ukijuwa hata ukimuacha hata huyo hawala yake hataweza kuendelea nae,maana wote wa wizi,nae huyo bwana ana mke wake pia...Kwa hiyo wewe ukimuacha ni adhabu kali kuliko hiyo ya kumkatisha maisha yake na yako pia... dhambi zake zote unambebea. .na Je unaporejea kwa Mola wako utamshitakia vipi huyo alo kuwa mkeo?..Kwanini usitafute mrembo mwingine ukaowa kuamuacha huyo akitangatanga mitaani..ni adhabu ya kumtosha hiyo na kwa Mungu akisubiriwa ....sielewi hiki kitu..kimekaa vipi..au dalili za Kiyyamah wanao tenda hawajijui SHETWANI KATANDA ULIMWENGUNI
ReplyDeleteSawa sawa. Mdau hapo juu. Mke mnzinzi achana nae. Kaoe mwengine ni kheli kuoa mwengine kuepukana na kama haya ya kuangamizana. Unamuacha kama mume au mke aendelee na uzinzi wake. Ndoa ni makubaliano tu ya watu wawili na mikataba ya maisha ili muishi pamoja kwa amani na upendo.Hata hao. Wasioachana wanasema ni huku huku kwetu Africa . Huko ulaya ndoa zinachana kama kawaida hiyo sheria ya kutokuachana mambo yenyewe kama hivi hawataki kabisa wazungu. Mke au mume akimshika ugoni na ndoa hamna inavunjika kwa kupeana talaka kufwata taratibu za kisheria. Baada ya muda makalatasi ya kuachana yamekamilika. Bwana anarusiwa kuoa au bibi kuolewa tena na mume mwingine. Tena ugoni hawana nao taraka rejea. Ugoni bibie au bwana ni kwaheri.
DeleteKwa imani ya kikristo kilicho unganishwa na Mungu hakuna wa kutenganisha kwahiyo hata ukimwacha mkeo/mmeo ukitoka na mtu mwingine ujue unazini, dhambi ipo pale pale ni mambo magumu sn hasa linapokuja suala la imani
ReplyDeleteDuuu ni hatari tupu.bora usiowe wala kuolewa basi.
ReplyDeletehatari tupu kwa sasa...
ReplyDelete