Vijana ishirini kutoka Shimoni Mombasa nchini Kenya wapo mkononi mwa idara ya uhamiaji mkoa Kaskazini Pemba baada ya mashua walio kuwa wakisafiria kutoka Mombasa kwenda Unguja kuharibika wakiwa baharini na kulazimika kujiokoa kwa kupitia bandari bubu ya Gando katika wilaya Wete.
Kiongozi wa mfara huo Willy Mwandwa na wenzake Kizito Bombo na Hanru Makau wamesema walilazimika kuingia kisiwani Pemba kwa kutumia bandari bubu na kujikuta wapo mikononi mwa vyombo vya ulinzi na usalama kutokana na kuharibikiwa na mashua yao waliokuwa wakisafiria kutoka Mombasa kwenda Unguja kufanya kazi katika kambuni yao ya ujenzi ilioko huko na kudai wao ni wasafiri halali hivyo wameshangaa kukamatwa.
Kwa upande wake Afisa wa Uhamiaji mkoa Kaskazini Pemba amesema wamewakamata vijana hao kucheki kama wana paspoti za kuingilia na endapo watajiridhisha kuwa wana vibali wata wachia kuendelea na safari yao na kuwataka watu wanao ingia au kutoka kisiwani pemba kuacha tabia ya kutumia bandari bubu.
Polisi Idara ya Uhamiaji inawashikiria vijana 20 Raia wa Kenya kwa kutumia Bandari Bubu kusafiria
0
April 10, 2016
Tags