Rais John Pombe Magufuli Amtumbua Jipu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji TIC


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Bi. Juliet Kairuki kuanzia tarehe 24 Aprili mwaka huu.


Taarifa iliyotolewa na kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda, imesema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya rais Dkt. Magufuli kupata taarifa kuwa Mkurugenzi huyo alikua hachukui mshahara wa serikali tangu alipoajiriwa mwaka 2013 jambo ambalo linazua maswali mengi.


Aidha, taarifa hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu huyo imeongeza kuwa endapo Bi. Kairuki atakuwa tayari kuendelea kufanyakazi na Serikali ya Awamu ya Tano atapangiwa kazi nyingine. Mchakato wa kumpata Mkuregenzi mpya umeanza mara moja.


Kwa mujibu wa Prof. Mkenda kwenye taarifa yake hiyo amesema Bw. Clifford Katondo Tandali, atakaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho cha Uwekezaji nchini TIC.
Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sasa kama hataki kupokea mshahara ndio atumbuliwe ? kwanza hii familia ya kairuki haina njaa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Aishije bila mshahara

      Delete
    2. Hataki mshahara lakini POSHO KIBAO,na hilo ndi tatizo.

      Delete
  2. mmh sio hivyo kuna mengine,si mseme ukweli.

    ReplyDelete
  3. SINEMA KILA SIKU TUMECHOKA, VITU VINAZIDI KUPANDA BEI, MAISHA MAGUMU MPAKA LINI TUMECHOKA NA SIASA HIZI

    ReplyDelete
  4. Mmechoka wakati mmemchagua wenyewe?ccm inawenyewe si ndio nyie mlikua mnaimba?

    ReplyDelete
  5. Na bado magu wanyooshe miika kumi ijayo watakua wametuliza akili hawatakurupuka

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad