Rais wa Serikali ya Mapinduzi wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein amesema kuwa kwa mujibu wa Katiba hakuna chama kilichokidhi masharti ya kuunda serikali ya Umoja wa kitaifa hivyo serikali ya visiwa hivyo itakua ni ya chama cha Mapinduzi.
Akizungumza katika Uzinduzi wa Baraza la tisa la Wawakilishi la Zanzibar Rais Dkt. Shein amesema kwa mujibu wa Katiba aliamua kumteua balozi Seif Ali Idd kuwa makamu wa pili wa rais ili kuunda serikali visiwani humo kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo.
Dkt. Shein amewahakikishia wajumbe wa baraza la wawakilishi kuwa serikali atakayoiunda itasimamia misingi ya haki, uwajibikaji,haki, uwazi na usawa wa wananchi wote bila kujali itikadi zao.
Aidha Dkt. Shein amesema kuwa katika kipindi atakachokaa madarakani ataendelea kuulinda Muungano wa serikali mbili wa Tanganyika na Zanzibar uliasisiwa tangu mwaka 1964.
Dkt. Shein ameongeza kuwa atahikikisha serikali hizo mbili zinafanya kazi kwa umoja na ukaribu zaidi katika kupanga na kutekeleza mikakati ya kiuchumi kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania wote.
Aidha amesema kuwa kwa kushirikiana na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema watadumisha Umoja na amani iliyopo visiwani humo huku akikisitiza kuwa maneno yanayotolewa na wapinzani hayamnyimi usingizi.
Muongo unakosa kwa dhulma ulowafanyia wazanzibari.
ReplyDeletemadaraka matamu babu kajishushia heshima yake
ReplyDeleteuso wake hauna furaha wala ukunjufu then anajionee aibu hana la kufanya dhulma imemzonga halali huo usingizi haupati na mgonjwa kula hawezi. asubiri ya salmini hapo chezea dua zinaanza kufanya kazi. mmoja mmoja.
ReplyDeleteyeye aliposema hakuwa na hekma wala hakujali je sie
ReplyDelete