Hatimaye Sakata la Uvumi na madai ya kijana,Nyabongo Manosa,ambaye inadaiwa alikufa kwa Malaria mwaka 2013 na kuzikwa na baadaye kudaiwa kuonekana hai katika kijiji cha Iroganzala,Wilayani Mbogwe Mkoani Geita mwaka 2015 limechukua sura mpya.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga Mponjoli Rotson,
Kwa Mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Rotson amesema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya Polisi kwa kushirikiana na mamlaka zingine ikiwemo ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serkali kuazisha na uchunguzi wa kisayansi ili kubaini ukweli juu ya marehemu anaedaiwa kuzikwa na kufufuka.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga Mponjoli Rotson, amesema Uchunguzi huo unafanyika kupitia jalada la uchuguzi Namba MB/IR/867/2015 liliofunguliwa kuchunguza tuhuma za vitendo vya ushirikina ambapo Uchunguzi utahusisha pia Vinasaba vya DNA.
Aidha katika kesi hiyo Polisi inamtafuta Bw. Emanuel Mutabo[ 42]anayehusishwa na tukio hilo anatafutwa baada ya kutoweka kusikojulikana toka Septemba 14 mwaka 2015 toka nyumba yake iliyolindwa na Polisi kutovunjwa na wananchi.
Kamanda Rodson amesema Nyabongo Manosa [19]alionekana 14 Septemba 2015 katika hali inayohusishwa na mazingira ya kishirikina maarufu kama MSUKULE ikiwa na maana ya mtu anayedaiwa kufariki na kisha kufufuliwa kwa ajili yakutumikishwa katika kazi za shambani na nyumbani.
Kamanda Rotson amesema Baada ya tukio hilo mtu mmoja aliejulikana kwa jina la Manosa Benjamini, mkazi wa kijiji cha Shinyanga A katika kata ya Nyakafuru wilayani Mbogwe alijitokeza akiwa na mkewe na kudai kuwa marehemu aliedaiwa kufufuka alikuwa mtoto wao aliyefariki kwa Maralia june 7 na kuzikwa june 8, 2013 katika kijiji cha Mpunze wilayani Meatu.
Mkuu huyo wa polisi amesema kuwa Bw. Manosa Benjamin, alikabidhiwa kijana huyo kupitia Ofisi ya Ustawi wa jamii wilaya ya Mbogwe, ili kuishi naye wakati uchunguzi wa kina ukiendelea kwani hapakuwepo na uthibitisho wowote wa kisayansi uliofanyika hatua ambayo imeendelea kuibua Uvumi na hofu ndani ya jamii.
Kukamilika kwa uchunguzi huo unaotarajiwa kukamilika ndani ya wiki mbili kutoka sasa kutahitimisha hofu na Uvumi wa tukio hilo ambalo kila kunapokucha limekuwa likiibua hisia tofauti ndani ya jamii bila kupata majibu ya kiuhalisia.
Sakata la Kijana Aliyefufuka Baada ya Kufa Lachukua Sura Mpya
0
April 05, 2016
Tags