Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salim amesema anakerwa na mastaa wanaodaiwa kuwa na tabia chafu zenye viashiria vya usagaji.
Shehe huyo aliyasema hayo hivi karibuni baada ya kutafutwa na gazeti hili kufuatia kusambaa kwa picha mitandaoni zinazomuonesha mwigizaji Wema Sepetu ‘Madam’ akiwa kwenye pozi la kimahaba na mwanamuziki Diana Exavery ‘Malaika’.
“Vitendo hivyo vinavyoashiria tabia za usagaji ni machukizo kwa Mwenyezi Mungu, pia ni laana na havikubaliki kabisa katika imani yeyote, anayefanya vitendo hivyo anatakiwa kuachana navyo maana havimpendezi Mungu.
“Wasanii wote, wanapaswa kutambua kuwa wao ni kioo cha jamii na watu wanahitaji kujifunza mambo mengi mazuri kutoka kwao na si kuwapotosha,” alisema Shehe Alhadi.
Ikumbukwe kuwa hii si mara ya kwanza kwa Wema Sepetu kujianika akiwa kwenye mapozi ya kimahaba na wanawake wenzake, alishawahi pia kuonekana katika pozi tata na mwigizaji Aunt Ezekiel.
Nikweli unachokisema hii si tabia nzuri,lkn nawy shekhe gani ambaye upo mpk kwenye mziki,hv hujui km muziki pia ni kitu ambacho kinakwenda kinyume namaadili ya dini yetu.jiangalie ww unaejiita shekhe kutumika kwako kunapiliza mipaka....tafakari
ReplyDeleteUsagaji upo Kila mahali duniani
ReplyDeleteTangu ikulu , makanisani, misikitikini
Hata Pope kasema
Kwani huyu sheikh ni mwanamziki?na una uhakika wa jambo hilo mpaka umamuanika mtandaoni?
ReplyDeleteLkn ni kharamu
ReplyDeleteAllah amewalaani wote wenye kusagana na kufirana
ReplyDeleteMxuuu mpaka wema atajwe
ReplyDelete