Sheikh Ponda akosoa utendaji wa Rais Magufuli..'Utendaji wa Rais Magufuli ni wa Kulipualipua'

SHEIKH Ponda Issa Ponda, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, amekosoa utendaji wa Rais John Magufuli, hasa dhana ya kutumbua majipu, akisema ina kasoro za kiutawala.

Akizungumza leo, Sheikh Ponda amesema utendaji wa Rais Magufuli ni wa kulipualipua.

“Ni kweli kwenye serikali kulikuwa na matatizo mengi, lakini lazima utaratibu kamili wa kuchukulia watu hatua ufuatwe,” amesema na kuongeza:

“Huwezi kuchukulia hatua watu bila kuwa na ripoti ya kitaalamu. Huko ni kufanya kazi kwa kulipuka.

Watanzania watafurahi zaidi kama serikali haitaingia hasara kutokana na kazi hiyo iliyo na shaka katika utekelezaji wake.”

Amesema ingekuwa bora kwa Rais Magufuli kusubiri ripoti za wataalamu wake, na si ‘kutumbua majipu’ kabla ya kupata ripoti.

Anasisitiza, “Jambo hili halipo sawa hata kidogo.”
Anasema dhamira ya kurejesha nidhamu serikalini ni nzuri na inahitajika sana, lakini namna ya utekelezaji wa dhamira yake hakuuanza vizuri.

“Juzi Rais Magufuli amepokea ripoti kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Angepaswa kuanza kuifanyia kazi ripoti hiyo ili kuepuka madhara kama yale ya kukamata meli ya uvuvi kwenye Pwani ya Dar es Salaam mwishowe serikali ikaingia gharama,” amesema Sheikh Ponda.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. na mimi pia nilikuwa na wasiwasi huo kuwa magufuli anafanya uamuzi wa haraka sana bila kufanya uchunguzi au ripoti yeyote, lakini hamna rais aliyefanya wema kwa watanzania kama Julius Nyerere, yule Jakaya Kikwete hakufanya kitu chochote kwa kuisaidia Tanzania, mimi ninavyomkumbuka Jakaya Kikwete ni safari zake kwa kwenda Marekani tu, simkumbuki kwa kitu kingine

    ReplyDelete
  2. Huyu julias nyerere ndio rais aliyeifanyia ubaya tanzania kushinda rais wote, kuanzia 1,mfumo mbovu na wa upendeleo wa elimu 2, kufuata siasa ya ujamaa na kuacha Sera ya viwanda 3,kutojali maslahi ya wananchi mfano mishahara,afya (hospital) nk 4,miundo mbinu yapo mengi tu Yaani huyo nyerere ni zero hata mkijaribu kumbeba mtaishia kusema kiswahili na amani utafikiri kabla yeye kuja dar kutoka butiama kulikuwa na vita kifupi nyerere ndio aliyechimba shimo tunalo jaribu kutoka kikwete ni kama mkaba tu Kala chake kaondoka

    ReplyDelete
  3. Tatizo raisi aliepita hakukaa vizuri kwa masrai au mustakabali wa Taifa. Yeye alikuwa na cheo cha juu kabisa lakini wajibu wake alikuwa haujui. Akachia nchi kama inajiendesha yenyewe hana hata habari ndio maana kila mtu akawa anafanya anavyotaka. Maadili ya nazi na sheria yote yakapuuzwa.nchi ilikuwa inaelekea pabaya sana. Na kukazuka wenye nacho na masikini. Na ingefika pahari masikini asingejaliwa tena angendelea kupuzwa na kuonekana kama si binadam. Na shida na dhiki zingendelea kwa kundi la masikini. Kila atapoitaji huduma muhimu angepuuzwa na kubezwa. Raisi anayoyafanya leo ni kutokana na misingi na tabia zilizojengeka kwenye miongozo iliyopita. Uongozi uliopita si kazi rahisi ni kazi ngumu. Kwani ilisha kuwa sehemu ya utamaduni wao baadhi ya watu na ni hatari kwa mustakabali wa Taifa

    ReplyDelete
  4. alipokuwa Nyerere kulikuwa hamna rushwa kama Kipindi alivyokuwa Jakaya na hata polisi wakaacha kufanya kazi au kuwa kazini,mpaka wezi wanauliwa kwa kupigwa mawe na kuchomwa moto, sababu wezi wakifikishwa kituoni wanatoa rushwa kwa polisi wanaachiwa baada ya siku mbili wanarudi mitaani kuwaibia watu, kama polisi wangefanya kazi kuwafunga wezi hao mauaji yasingetokea yaani wakati wa Jakaya watu walikuwa hawafanyi kazi mpaka daktari mkuu hospitalini walikuwa wanaenda kunywa pombe wakati wa kuwa kazini, na Jakaya mwenyewe alikuwa kila mara yuko Marekani hata baada Tanzania kupata rais mpya Jakaya bado akaendelea kwenda marekani.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad