Sijawahi Kutoka na Nisha na Wala Hajawahi Kuwa Hata Mshikaji Wangu -Baraka de Prince

Msanii Baraka de Prince ambaye kwa sasa anafanya poa na ngoma yake ya 'SIWEZI' na ambaye amedondoka kwenye penzi la msanii mwenzake Najma Datan amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake yeye hajawaji kutoka kimapenzi na msanii wa filamu

Akiongea kwenye kipindi cha Friday Night Live, Baraka de Prince alisema kwamba yeye hajawahi hata kuwa na ushikaji na msanii huyo na kusema kwamba inawezekana ni shabiki mzuri wa kazi zake ila hajawahi kutoka nae kimapenzi kama ambavyo inazungumzwa mtaani na kama ambavyo msanii huyo alivyowahi kusema kuwa anatoka na Baraka de Prince.

Mbali na hilo Baraka de Prince alizungumzia juu ya show kubwa ambayo ataifanya siku ya kesho Jumapili pale Coco Beach kwenye show iliyoandaliwa na East Africa Radio kwa ajili ya kushererekea miaka 17 toka imeanzishwa. Ambapo Baraka de Prince amesema ni show yake ya kwanza kubwa kufanya hivyo amejipanda kuwapagawisha wana ambao watatokea,

"Unajua mimi ni msanii wa mtaani na watu wangu wengi wa mtaani huwa wanashindwa kuibuka kwenye show zetu hizi za Club na sehemu zingine ila naamini show ya kesho wataibuka wengi halafu mimi nitaimba nao mwanzo mwisho, sababu mimi ni mtu wao".
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. lakini wasanii wa kike kwa nini mnakubali muumbuliwe na wanaume namna hiyo unatembea na mtu halafu anakuja kukukana, mambo hayo yamemtokea Jokate japokuwa Jokate ni mrembo mkali lakini ali kiba alisema hakumpenda Jokate alikuwa naye sababu ya kazi tu, mimi ni msichana wa kibongo naishi Ulaya na wala sikubali mwanaume anifanyie upuuzi kama huo halafu niandike kwenye social media kuwa natembea na mwanaume fulani. Hata siku moja, ona sasa wasichana umnavyokanwa na wanaume, wanawakana kabisa ni aibu.

    ReplyDelete
  2. Halafu wewe Nisha ni mrembo sana kuliko huyo Baraka de prins hana hata sura halafu anakuaibisha, na pia Ali kiba alimuabisha Jokate wakati Jokate ni mrembo sana kumzidi Ali kiba hana hata sura halafu Ali kiba hajui hata kuvaa vizuri. Diamond anamzidi Ali kiba kwa kuimba na mavazi, Diamond yuko Ulaya na mimi naishi Ulaya nitaenda kumwangalia Diamond, lakini kama angekuja Ali kiba kuimba Ulaya nisingeenda kumwangalia akiimba, na alishawahi kuja Ulaya miaka ya nyuma kuimba wala sikwenda kumuangalia Ali kiba, mimi naona katika wanamuziki wa kibongo ni Diamond tu anaimba vizuri, lakini Alikiba tupia kule kwenye jalala

    ReplyDelete
  3. hivi huyu Baraka da Prince yeye aliingia kwenye game la music kwa ajili ya kupata wanawake au kufanya maisha maana wenzake wanaongelea maendeleo ya maisha yeye kila leo ni scandal za mapenzi tu hata akiongea ni kujisifu tu kuhusu wanawake kwa staili atafeli tushachoshwa na huyu mshamba wa umaarufu anatuabisha watafutaji duh

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad