Siri ya Rais Magufuli Kuchagua Kutembelea Nchi ya Rwanda na Kusafiri Kwa Kutumia Usafiri wa Gari Hii Hapa

Tusihangaike Na Kwanini Magufuli Kachagua Rwanda Kama Nchi Ya Kwanza Kuzuru...
Tujiulize, Magufuli aliyekwenda kwa Kagame kwa barabara akirudi atakuwaje?
Ndugu zangu,

Wahenga walisema, tembea ujionee, ina maana tembea ukijifunza. John Magufuli anajenga ubia na Paul Kagame. Urafiki wa John na Paul, na atakayojifunza John kwa rafiki yake Paul, yumkini yataongeza maradufu kasi ya John Magufuli kutumbua majipu.

Kagame pamoja na kuitwa dikteta, lakini ameibadilisha Rwanda na inaelekea kuwa nchi ya kisasa zaidi. Siri kubwa ya mafanikio ya Rwanda ni kwa Kagame kuwafanya Wanyarwanda kuheshimu sheria, kanuni na taratibu za nchi. Kujenga misingi ya uadilifu na kuisimamia. Na wenye kukiuka kuadhibiwa. Ni kwa viongozi na raia.

John Magufuli ameanza kuijenga misingi hiyo hapa nyumbani, na kwa atakayoyaona kwa rafiki yake mpya Paul Kagame kule Kigali, basi, John Magufuli njiani akirudi nyumbani atakuwa akijisemea.
;" Yaani, kaanchi kadogo aka ka rwanda, hakina hata bandari wala migodi ya madini katupite hivi hivi kwa vile sisi tumekubali kuyafuga mafisadi...uwiii!"
Goodmorning.
Maggid.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwa kwel Kagam na mimi namkubal kwa yal aliy yafany, ila jamaa huyuu kam humjui uliz utaambiwa Kagame ni nani? jifunzen kutok Burundi kwa rais Puere Nkurunziza apo awali walikuaje na Kagame? na sasa wako vipi? Museveni na Kagsme walikua vip na leohii wako vipi? jifunzen kutok Burund na Uganda kabla ya kusifia uhusiano wa Tanzania na Rwanda.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad