Sugu
Rapa huyo ambaye aliachia wimbo ‘Freedom’ ambao unafanya vizuri kwa sasa, ameiambia Bongo5 kuwa wakati ndio umesabisha soko la albamu kupotea.
“Sisi Tanzania nafikiri tuliwahi kuingia kwenye biashara ya albamu, wenzetu Jamaica wasanii wakubwa kwao, yaani nyumbani kwao Jamaica hawauzi hata nakala elfu 10000, labda wawe International ndio wanaweza kuuza zaidi kazi. Lakini kule kwao ndani waliwekeza kwenye show zaidi na matamasha. Sisi tulianza na albamu bila kuboresha matamasha, na watu wakatuacha huko huko tunagombana na Waindi, na huku show kwa sababu hatukutolea macho wakawa wanatulipa pesa ndogo, kwa sababu tulikuwa hatujui show zina pesa nyingi. Kwa hiyo kilichotokea ni kama mabadiliko, tulianza na ambako pengine hatukutakiwa tuanze, na sasa hivi nyakati imeturudisha pahala ambapo tunatakiwa kuwepo,” alisema Sugu.
Pia alisema kwa sasa mataifa makubwa ya ulaya ambayo yameendelea kiteknolojia wameanzisha mifumo mipya ya kuuza albamu ambayo inawapa pesa nyingi.
Chanzo:Bongo5