Nimeileta hii mada huku kwa makusudi kwakuwa inahusika na mapishi lakini vile vile na afya zetu kwakuwa mapishi na afya haviachani
Sehemu kubwa ya mboga za Darisalama zinatoka mabonde ya Mto Msimbazi, Mandela road bonde lililoko kituo cha garage, Jangwani, Kigogo sambusa na maeneo ya Tandale na kwingineko
maji yanayopita kwenye mabonde haya ni machafu, yenye kemikali toka viwandani, yenye vinyesi toka vyooni nk ndio hayo hayo yanayonyweshea mbogamboga hizi tangu kuchipua hadi kukomaa.
Kwa vyovyote vile, maji haya yakipimwa ni wazi yatakutwa na kiwango kikubwa cha sumu mbalimbali zinazosababisha magonjwa kansa na ngozi.
Uchafu tunaoutupa kwenye mito ipitayo kwenye haya mabonde kama betri za simu na magari material za friji mbovu, computer mbovu nk nk vyote hivi vimebeba kemikali zenye sumu kali.
Tusipochukua tahadhari tutaishia kuongeza vyumba pale Ocean road kwenye ile hospital ya kansa
By Mshana JR/Jamii Forums
Mmmh
ReplyDelete