Ni ukweli kuwa uhusiano wetu na Kenya haujawahi kuwa wa "mahaba" (tukitumia msemo wa Lowassa). Tumekuwa tukivumiliana kwa maslahi ya kiuchumi tangu enzi za mwalimu. Hata hivyo tangu awamu ya tano ianze uhusiano wetu na Kenya unatia mashaka na ni vema tukaongelea jambo hili objectively.
Mambo yalianza na Magufuli kuchaguliwa kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM. Ikaelezwa viongozi wa serikali ya Kenya walipata hofu kwa vile Magufuli ana urafiki na kiongozi wa upinzani.
Likaja suala la njia ya Bomba la Mafuta. Magufuli akaongea na Mseveni na kukawa na uwezekano mkubwa kuwa Uganda itachagua njia ya Tanzania badala ya Kenya. Suala hili halikuifurahisha Kenya hata kidogo. Kwa sababu ya ushindani wa njia ya bomba la mafuta wakati fulani waziri mmoja wa kenya na maafisa wake walizuiliwa uwanja wa ndege Tanga.
Jambo jingine la kuchekesha ambalo wakenya waliandika ni wakati wa mkutano wa marais wa EA ambapo Magufuli aliongea ki-luo mbele ya Kenyatta. Media ya Kenya ikachukulia ni kejeli kwa Kenyatta kwa vile rafiki wa Magufuli ni M-luo.
Tukio jingine dogo ni la binti wa rafiki mkubwa wa Magufuli kusema kuwa Olduvai Gorge iko Kenya. Media ya Tanzania ikalipuka kwa kulaani. Hii inatokana na historia ya Kenya kuitangaza Kilimanjaro kuwa iko kwao.
Katika mtazamo huohuo juzi wakati anafungua Daraja la Nyerere (Kigamboni) Rais Magufuli aliwasha moto mwingine kwenye media ya Kenya kwa kusema "wale wanodhani kila jambo jema liko kwao wameanza kuandika...walisema Kilimanjaro ni yao, Olduvai Gorge ni yao, n.k" . sasa hivi hii kauli iko katika headings za media za Kenya: "Magufuli fires shots...", "Magufuli hates Kenya with a passion"...n.k
Posts za wakenya kwenye blogs na online newspapers sio positive kama mwanzo wakati Magufuli kaingia madarakani. Watu wanatutukana. Wanauliza tuna nini zaidi ya Kiswahili na hili daraja la Kigamboni. Wanaona serikali ya Magufuli imedhamiria kuifanya Tanzania iwe Juu ya Kenya.
Kuna umuhimu viongozi wetu kwa makusudi wafanye bidii ya kuondoa hii hali ya vita ya maneno. Ile tabasamu Magufuli na Kenyatta wanaonyesha wakikutana iwe pia tabasamu kati ya watu wetu na media zetu.
UMEKOSA CHA KUANDIKA?
ReplyDeleteWaandishi mmekuwa wachochezi pia.
ReplyDeleteAcheni kukuza mambo nyie waandishi.
ReplyDelete