Jeshi la Polisi Zanzibar limefanikiwa kuwakamata watu wanne wakiwemo vigogo wa Chama cha Wananchi CUF wakituhumiwa kupanga na kuhusika katika uratibu,utengenezaji na ulipuaji wa mabomu kisiwani Zanzibar.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Naibu Mkurugenzi wa upelelezi na Makosa ya Jinai Zanzibar Kamishina Msaidizi wa polisi Salum Msangi amesema watuhumiwa hao wamekamatwa baada ya upelelezi wa kisayansi wa Polisi huku akisema wengine ni viongozi wa juu wa CUF na wasomi na wataalamu wa Chuo Kikuu cha Zanzibar ambapo lengo lao likuwa ni kulipua makazi ya Makamu Wapili na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar .
Watuhumiwa waliokamatwa ni Omar Bakari Nassor,Hassan Omar Issa Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Magharibi Salehe Mohamed Saleh Katibu wa CUF Magharibi na Suleiman Mohmaed Bakari Katibu wa CUF Mfenesini.
Mkuu huyo wa upelelezi amesisitiza na kutoa onyo kuwa Jeshi la Polisi halitasita na linaendelea na kazi ya kuweka ulinzi kwa wananchi na yeyote au kikundi kitakachojaribu kuleta fujo polisi imejiandaa kikamilifu.