Wajapan Waikopesha Tanzania Mabilioni ya Fedha



Shirika la maendeleo la kimataifa la Japan (JICA) na Wizara ya Fedha na Mipango wametiliana saini mkataba wa mkopo kutoka Japan kwaajili ya mradi wa maendeleo wa kuimarisha mazingira ya biashara na uchumi nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar Mkurugenzi Mtendaji wa JICA Toshio Nagase amesema mradi huo unahusisha mfululizo wa mageuzi ya sera za maendeleo ambao utaweza kuondoa vikwazo katika mazingira muhimu ya biashara nchini hasa katika viwanda na sekta zinazotoa ajira.

Mradi huo utashughulikia maeneo makuu yenye vikwazo kwa kurahisisha usajili wa biashara na upatikanaji wa leseni, kuimarisha ufanisi na umahiri wa utawala wa forodha hasa katika bandari ya Dar es salaam , kuboresha ufanisi katika usimamizi wa kodi, kurahisisha mchakato ywa usajili wa ardhi, kuboresha upatikanaji wa fedha za mitaji na kupunguza gharama za usafirishaji wa bidhaa za kilimo na mazao.

JICA imedhamiria kuunga mkono serikali mpya katika njia mbalimbali ili kuharakisha juhudi za serikali katika kuifanya Tanzania iwe nchi ya viwanda na ya uchumi wa kati kama ilivyoainishwa katika dira ya maendeleo ya 2025.

Mkopo huo una thamani ya fedha za kijapan billion 6 ambazo ni sawa na fedha za kitanzania shilingi bilioni 116 na mradi huo unafadhiliwa kwa pamoja na benki ya dunia.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad