Wasalaam, Wakati wa tawala zilizopita watanzania wengi waliulalamikia mfumo wa uendeshaji wa serikali chini ya chama cha mapinduzi. Wengi walisikika wakisema kwa mfumo huu hata aje malaika kutoka Mbinguni hakuna mabadiliko katika taifa letu.
Rais John Magufuli, tayari amebadilisha baadhi ya mambo hapa nchini na hata ule utamaduni wetu wa chukua chako mapema unaanza kuondoka taratibu.
Wale wenzangu mnasemaje sasa? Kwa sababu hata magufuli mfumo anaoutumia ni ule ule wa ccm
By Tawa
Kwani bado tupo kwenye kampeni?mbona ndio kwanza anaanza tusubiri basi na kampeni zimeisha kitambo.
ReplyDeletehahahahah! Unajisahaulisha sio??? Hilo ni dongo limetupwa gizani, atakaye sema 'yala' limempata. Waloambiwa hayo maneno wenyewe wanajijua, waliyasema hadharani bila kificho wala haya, tena kwa uhakika na kujiamini, hivi sasa wamebaki wadogo kama 'nukta', wamebakia kuulizia mara mshahara, mara posho za JPM, hawana jipya.........HAPA KAZI TU, MAJUNGU KWENU
ReplyDeleteSaafiii. Nadhani mbali na mtu, pia mfumo bado unahitaji kubadilika. tuangalie ya Zanzibar, Magufuli na uthubutu wake wote lakini pale ka fyata mkia, maana mfumo bado uko kazini. na ninaamini, katika mfumo huu uliopo, Magufuli hawezi kugusia swla la kiba mpya kabisa! ( nazungumzia katiba ya wanachiile ya Warioba, siyo ile pendekezwa) mana hiyo ndo kichaka chenyewe cha hao ma bwana kuondelea kuwepo madarakani. hiyo iking'oka tu. nchi tumeikomboa. Magufuli hana uthubutu huo. so my take ni kwamba mfumo bado ndo tatizo.
ReplyDelete