WOSIA wa Liyumba kabla ya Kifo Chake

Wosia huo wa Liyumba, ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Benki Kuu Tanzania (BoT), ulifanya waombolezaji waliofika kuuaga mwili wake, kutopewa fursa ya kuona sura yake kwa mara ya mwisho kabla ya maziko.

Ndugu huyo alitangaza utaratibu huo jana baada ya ndugu, jamaa na marafiki kufika nyumbani kwa marehemu kutoa heshima za mwisho.

Baada ya mwili kuwasili na taratibu nyingine kufanyika, Merito alisimama na kutangaza kuwa kaka yake aliacha wosia kwamba wakati wa kuagwa, ndugu pekee ndiyo wamtazame uso wake.

“Alisema watu wengine watakaoshiriki msiba wake, wapite kwenye jeneza lake likiwa limefunikwa,” alifafanua.

Baada ya utaratibu huo kutangazwa, waliofika kuaga walipita mbele ya jeneza hilo likiwa limefungwa na kutoa heshima zao za mwisho.

Aidha, alisema kutokana na taratibu za kimila, mwili huo ambao jana ulitangazwa utazikwa leo mkoani Morogoro, utaratibu umebadilika na kwamba atazikwa kesho.

“Mila zinasema mwili wa marehemu baada ya kuwasili Morogoro, unatakiwa kulala kwenye nyumba yake hadi siku inayofuata ndipo utaratibu mwingine wa maziko ufanyike. Kwa hiyo atazikwa Ijumaa (kesho),” alisema.

Miongoni mwa walioshiriki kwenye msiba huo ni pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa BoT.

Liyumba ameacha watoto saba, mkewe alifariki dunia miaka 10 iliyopita.

Enzi za uhai wake, alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwaka 2009 kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi na kuisababaishia serikali hasara ya Sh. bilioni 221.

Hata hivyo, alishinda kesi hiyo baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha tuhuma hizo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad