Zitto ‘Amchana Laivu’ Rais Magufuli..Adai Bado Hafanyi Inavyopaswa.......

ZITTO Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT- Wazalendo amesema, Rais John Magufuli anapapasa suala la ufisadi, anaandika Pendo Omary.

Amesema, serikali yake bado haijachukua hatua madhubuti katika vita dhidi ya rushwa nchini licha ya ‘shangwe’ nyingi.
Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa Halmashauri Kuu ya ACT- Wazalendo.

“Bado Rais hafanyi inavyopaswa, bado rais anapapasa suala la ufisadi. Kuna mambo ya muda mrefu ambayo tunaendelea kama nchi kuyalipua lakini arais ameyakalia kimya. Mfano ni suala la Tegeta Escrow,” amesema Zitto na kuongeza;

“Bado mtambo wa IPTL upo chini ya matapeli na kila mwezi serikali inawalipa matapeli hawa zaidi ya Sh. 8 bilioni wazalishe au wasizalishe umeme.
“Hivi ndio vikundi maslahi  katika sekta ya nishati ambavyo bila kuvibomoa, rais ataonekana anachagua katika vita hii.”

Zitto amesema, serikali imeficha inaowaita madalali wa rushwa katika suala la hati fungani ya Dola za Marekani 6 milioni.

Na kwamba, tayari kuna watu wamefikishwa mahakamani lakini  walioitoa rushwa hiyo ambao ni Benki ya Standard ya Uingereza na waliopokea ambao ni maofisa wa serikali, hawakupelekwa mahakamani.

“Hati fungani hii ambayo serikali imeanza kulipa riba yake ni ghali mno na imeongeza deni la taifa kwa kiwango cha Sh. 1.2 trilioni bila ya riba. Itakapofika mwaka 2020 ambapo tutakuwa tumemaliza kulipa deni hili, tutakuwa tumelipa zaidi ya Sh. 1.8 trilioni, shilingi bilioni 600 zaidi,” amesema Zitto.
Zitto amesema, Watanzania zaidi ya 2000 duniani kote wameweka saini kutaka Taasisi ya Rushwa kubwa nchini Uingereza ( SFO ) kufungua upya shauri hili na kuitaka Benki ya Standard iwajibike kwa ufisadi huu dhidi ya nchi masikini ya Tanzania.

Amesema Rais Magufuli angeongoza Watanzania kukataa mikopo ya namna hiyo ambayo inafukarisha nchi ingekuwa ni hatua kubwa lakini Taasisi ya Kupambana na Rushwa (Takukuru) wanaona sifa kuweka ndani watu kwa Sh. bilioni 12 bila kuwataja watu watakaofaidika na Sh. bilioni 600 zaidi zitakazolipwa katika deni hilo.

“Ndio maama tunasema rais na serikali yake bado hawafanyi ya kutosha katika vita dhidi ya rushwa. Sio suala la kutumbua majipu tu, ni suala la kuweka mfumo madhubuti ambao utazuia rushwa kabisa.

“Chama chetu cha ACT -Wazalendo ni lazima kiendelee kuunga mkono juhudi zozote za kuondoa ufisadi nchini kwetu. Hata hivyo chama chetu ni lazima kiendelee kukosoa serikali pale ambapo tunapoona mambo hayaendi sawa.

“Tusiogope kuikosoa serikali kwa hoja kwani kukosoa serikali ni tukio muhimu sana la kizalendo,” amesema Zitto.

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wewe Zitto Kwabwe..tulikuweka Kafika time za binge.. Cha. Maana ulichofanya Ni kipi ambacho Unaweza kujivunia kwamna hapa nimefanya la maama..au unajikumbusha Sitta alivyo. Kubalisha kilemba cha ukoka... Lets mawazo ambayo yatamsaidia mtanzania..na siyo kwa jinsi hii... Je unajua hii inatupelekea wapi?? Ni kuzua mijadala isiyo na msingi na kuleta maskando ambayo yatapoteza wakati na nguvu za watu ..kama watakusikiliza...mimi nakuomba si hapa wala so ndani ya binge letu na magenge yenu.. Magufuli is a man 👨 of action..He does not talk much. He evaluate the scene including a wider scenerio and next is action 🎬 plan.. Mchezo umekwisha..So his decision and when he takes including how..is non of your Business..au wewe uanze kumfundisha hapa ingefanya hivi..kama kweli tungekuchagua wewe..lakini sivyo ..tumemchagua yeye bila kutaka msaada au ushauri toka kwako..Zitto Una umuri gani hivi sawa?? Mwangalie JPJM Kwa mbali ukiweza msalimie lakini Kula mmoja na hamsini zake kwa kazi na majukumu yake.. Je wewe Ni yapi?? JPJM Tumemuamini na ametuahidi Hato tuangusha..nakuomba utulie na jukwa lako tutakutengenezea kunafi ssere zako!! Hiyo Ni kama unazo sera mpya.. Tumechoka na tabia za kuanzisha maskendo halafu watu wajipatie ulaji. Hatuyataki hayo...na haya ya nyanzo madudu madudu PIA hahaha mwelekeo .. Zitto karibu Kwenye Tanzania yetu mpya ..tuko ktk kuijrnga kama unataka kushiriki wacha huu mwendo WA kutuchelewesha..asili yake Ni uvivu. Umeipata Mwaya!! JPJM CONTINUE THE WAY YOU DEEM AS NECESSITY RATHER THAN... TUTAFIKA.. WENYE MANEMO MENGI MWISHO WAO UNAJULIKANA WAZI... POLE KAKA

    ReplyDelete
  2. Udaku..hivyo hiki kichwa cha Habari Mbona kinatisha?? Kabwe alinena a wapi haya??

    ReplyDelete
  3. Kweli Kabisa zitto
    Atumbuwe na marais waliomtangulia

    ReplyDelete
  4. Zitto . Mtukifu Raisi anayo list ya priority..PIA ujue kwamba anayo teamya watendaji..pia anao uwezo WA kudelegatw utendaji kwa anaye mtaka kwa janbo analolitaka na wakati anaotaka.. Kwa hhiyo badala ya kuUngimzza hio cabichi .. Vuta aubira na Matokeo utayaona wewe means siasa.. WA chama gani vile?? JPJM ...HAPA KAZI TUUUU

    ReplyDelete
  5. zito you are talking too much muachne RAINING afanye kazi yake ndio maana watanzania tumemchagua wewe kimbelembele cha nini tulia kaka uone matokeo tumechoka na scandal zako kila asubuhi unatusabahi na scandal tunataka amani wacha RAISI afanye uamuzi wewe mtoto wa juzi unaongea hadi una kerala tulia bwana

    ReplyDelete
  6. Anonymous WA April 26, 2016 at 6:52 PM, POLE SANA KWA KUTOYAPENDA MAONI YA ZITO KABWE. UNAONEKANA UNA AKILI SANA. KIINGEREZA CHAKO NIMEKIPENDA. ILA NAKUSHAURI TUMIA KISWAHILI ZAIDI HALAFU SOMA STORY YAKO KABLA HUJAPOST. PIA USIPOFUKE SANA MACHO KWA MIHEMKO YA KISIASA. ZITO ANA HOJA ZILIZOPANGIKA. UKISAHIHISHA VIZURI HOJA ZAKO UTAJITAMBUA.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad