Zitto Kabwe Afunguka 'Watumishi Hewa Kwenye Wizara Mbona Hatusikii? Najitolea Kutumbua wa Wizara ya Ujenzi'

Mbunge wa Kigoma mjini kupitia ACT wazalendo Zitto Kabwe, ameitaka serikali kuwabainisha wafanyakazi hewa kwenye wizara, baada ya agizo la Rais la kuhakiki watumishi hewa kwenye halmashauri kutekelezwa.

Zitto Kabwe ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake facebook, na kuonesha kushangazwa kwa wizara kutoweka wazi wafanyakazi hewa waliomo humo, huku akijitolea kubainisha wale wa kwenye wizara ya ujenzi.

“Watumishi hewa kwenye wizara mbona hatusikii? Wakuu wa mikoa wameagizwa kutambua watumishi hewa. Mawaziri hawakuagizwa. Ok ngoja nijitolee kutambua watumishi hewa wizara ya ujenzi kupitia ripoti za CAG 2010/2011 mpaka 2014/2015”, aliandika Zitto Kabwe.

Hivi karibuni mikoa yote nchini imetekeleza agizo la kuhakiki wafanyakazi hewa walioko kwenye halmashauri zao, huku mkoa wa Mwanza ukiongoza kwa kuwa na wafanyakazi hewa 334

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. WATAJE WATAJE!!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Anataka AIRTIME...NPENI SMATI PHONI AJISMATIDONISHE ..AU LAIVU KAVA..

      Delete
  2. we zito mbona hata jimboni kwako hatukuoni kazi kubwabwaja tu, ndo maana ulihama jimbo baada ya kuona mambo si mazuri usitafute kiki mbona mwanzo mlikuwepo lakini hatukuona kama mnalizungumzia hilo la watumishi hewa???? kama unawafahamu wataje

    ReplyDelete
  3. Huyu ndiyo yule WA Laivu kavarehi .na aokomoko katija Bunge. Hana jipya...TUMEXGOKA

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad