Zitto Kabwe Aibua Mazito Bungeni: Ukiukwaji wa Sheria ya Bajeti, Ufisadi wa Hati Fungani ya Sh1.2 Trilioni

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe jana aliibua mambo mazito bungeni wakati akichangia mjadala wa Bajeti ya Ofisi ya Rais –Tamisemi na Utawala Bora, likiwamo la ukiukwaji wa Sheria ya Bajeti kutokana Bunge kupitisha bajeti Sh23.7 trilioni huku Serikali ikija na bajeti ya Sh29 trilioni.

Mambo mengine yaliyobainishwa na mbunge huyo ni sakata la ufisadi wa hati fungani ya Sh1.2 trilioni katika Benki ya Standard ya Uingereza na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kushindwa kutoa majibu ya uchunguzi wa miamala kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow kwenda Benki ya Stanbic.

Tazama Video Hapa Zitto Akimwaga Cheche:


Kuhusu bajeti, Zitto alisema kuna ukiukwaji wa Sheria ya Bajeti namba 11 ya mwaka 2015 katika mchakato wa bajeti ya mwaka 2016/17 kwamba kifungu cha 8 cha sheria hiyo kinaeleza namna ambavyo mfumo wa bajeti ya Serikali unapaswa kuwa.

“Vifungu cha 8(1)(b) na 9(1)(a) na 19(1) vinataka ‘mpango na miongozo ya bajeti’ ipitishwe na Bunge katika mkutano wake wa Februari kila mwaka. Bunge lilikaa kama Kamati ya Mipango na kupitisha Mpango wa Bajeti uliokuwa na Bajeti ya Sh23.7 trilioni,” alisema.

Alisema kiasi hicho ni tofauti na bajeti inayojadiliwa sasa ya Sh29.5 trilioni na kubainisha kuwa jambo hilo si utawala bora kwa maelezo kuwa utungaji wa bajeti umeainishwa kisheria na kama sheria hazifuatwi, ni vigumu hata Bajeti yenyewe kutekelezwa.

“Ili kurekebisha hali hii ni lazima Bunge likae tena kama kamati ya mipango na kupitisha upya viwango vya juu vya bajeti kabla ya mjadala wa bajeti kuendelea au angalau kabla ya kupitisha bajeti kuu, Juni 2016,” alisema na kwamba bajeti za taasisi hazimo kwenye vitabu vya bajeti ya Serikali kinyume na sheria ya bajeti.

Kuhusu ufisadi wa Sh1.2 trilioni, mbunge huyo alisema mwaka 2013, Serikali ilikopa fedha hizo kutoka nje kwa msaada wa Benki ya Standard ya Uingereza ambayo sasa inaitwa Standard Bank, kwamba mkopo huo wenye riba inayoweza kupanda umeanza kulipwa Machi mwaka huu.

Alisema mkopo huo utalipwa mpaka mwaka 2020 kwa mikupuo tisa inayolingana na kuongeza kuwa mkopo huo umegubikwa na ufisadi huku baadhi ya Watanzania wakiwa tayari wamefikishwa mahakamani wakihusishwa na sehemu ya mkopo huo.

“Jambo la kushangaza ni kwamba wanaosemekana kula rushwa hiyo hawapo mahakamani mpaka sasa. Vilevile, waliotoa rushwa hiyo hawapo mahakamani mpaka sasa. Waliopo mahakamani ni wanaosemekana kutumika kupeleka rushwa. “Mjumbe kashtakiwa, lakini aliyemtuma hajashtakiwa na aliyepelekewa kilichotumwa hajashtakiwa. Hapa kuna tatizo la msingi ambalo tukilitatua Serikali yetu itaepuka masuala kama haya siku za usoni.”

Alisema ana barua ya kundi la Watanzania zaidi ya 2,000 wakitaka benki hiyo ya Uingereza ichunguzwe katika suala hilo la hati fungani huku Takukuru ikitumia taarifa ya Taasisi ya Uingereza ya (SFO) katika kuchukua hatua zinazostahili dhidi ya Watanzania wanaotajwa katika sakata hilo.

Alisema SFO haikufanya uchunguzi dhidi ya benki hiyo ya Uingereza na kushangazwa na Tanzania kusaidiwa kesi hiyo na wataalamu kutoka nchi hiyo.

“Iwapo tutafanikiwa kuonyesha kuwa Benki ya Standard ilihonga kupata biashara nchini kwetu, Tanzania itakuwa fundisho kwa kampuni ya kimataifa kwamba Afrika siyo mahala pa kuhonga na Tanzania haitalipa mkopo huu na riba zake na tutaokoa zaidi ya Sh2 trilioni katika deni la Taifa,” alisema.


Chanzo: Mwananchi
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Zitto..Bunge letu tukufu Ni la kujadili Sheria/ Mipango ya maenndeleoo na. Huruma zza jamii zinazo mbana mwananchi WA kamaida mjini na vijijini . Hii Ni kwa taarifa yako na ukumbusho ... Hoja zako na sera zako za kipelelezi na maskendo kama unavyo eleweka ningekuomba uwe unapeleka sehemu husika ambapo utasikilizwa na hatua za haraka zitachukuliwa kudeal na huo qizi huko polisi na mahakama ikifatia wajini hizo ruhuma na tutakupa wakili WA serilali na mwendesha mashtala..hilo tunakuahidi ..lakini kutuinia muda wetu bungeni kuleya skendo na watu wanakupigia makofi Baba akaleta skendo mpya..hatutaki..MHK.Majaliwa nakuomba ulifupishe Hilo..na spika wetu alifanyie awareness kwa wabunge..HII AWAMU NI YAKUMTUMIKIA MWANANCHI NA NCHI SIITYO YA KUANZOSHA TUME NA VIKAO KUKOSESHA UCHANGILIAJI WA MAENDELEO YETU... POLISI IPO NA NINAIMANI UTASIKILOZWA NA WATALIFANYIA KAZI LOLOTE KAMA LINAUKWELI..USIYULEYEE HAYA KUFFIRAHISHA VIKINDI NA KUOMDOA MANTILI NA MAUDHUI YA BUNGE... UNANIELEWA ZIZURI NAKUOOMBA UTAFAKARI..ASANTE USITICHOSHE MWANANGU... BUSARA NA UVUMILIVYO NI VYA MAANA.. AJIRA IPO NA WAHISIKA WANATOA USHIRIKIANO

    ReplyDelete
  2. We AnonymousApril 30, 2016 at 10:40 AM huna akili kabisa
    Pumbafuuuu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe simuone kama unamwonaga mupumba huyu nchemba so muambiage umsaidiage kumqereweshaga upumba..rabuda anasemaga ramana. We simuone yerezaga tu.. Kwanaga unakieaga wewe Tu pimbi..tumechogaga na zitto hatakagi kuerewaga Tukuliru na porisi mirangi iko wazi.. Siyo kubungeretu ...nzee Ndungai anamengi ya maama kurikoni

      Delete
  3. Zitto tunafurahi unapokuwa unaweza kuona mambo ambayo sisi wengine hatuyaoni au kuyajua.. Je wewe kama mzalendo mkereketwa na haya... unachukua hatua gani zaidi ya kuyafikisha bungeni ili uendeleze sokomoko zinazoendelea na kupewa vichwa vya habari na media visivyo stahili.. Mimi kukuona wewe kuwa ungeweza chukua hatua katika sehemu husika kama vile TAKUKURU / POLISI / MWANASHERIA NA MUENDESHA MASHTAKA... Hawa watu hizi ndiyo Role zao ambao wanatambulika kisheria na wao kuwajibika katika hoja yeyote utakayo wapelekea ninaimani Kazi watalifanyia ili mradi imethibitika hivyo na Mabalozi wetu watachangilia ufatiliaji katika nchi husika na ikibidi tutafanya international arbitration agreed between our involved countries.. Zitto wacha bunge letu na wananchi kuwapa fikra za sivyo ndivyo... Magufuli ameona mianya na anaishughulikia.. lakini usidhani kwamba ni rahisi atamaliza kwa siku au mwezi.. anazo list za priority naomba uwe na imani hiyo.. wewe pia unaweza kumtembelea Mh Majaliwa mlango wake uko wazi. na atakusikiliza na kazi atayafanyia bila kuwawe katika njia unayoa mua wewe.. sisi sote tunataka kuiona Tanzania mpya ya maendeleo na siyo ya siasa nyingi.. japo mnataka kuleta siasa katika haya... ndugu zangu sivyo hivyo... Maendeleo ni ya watanzania na sivyo ya wafuasi wa vyama.. KARIBU tAKUKURU / KARIBU pOLUA NA TISI/ kARIBU OFFICE YA W/MKUU.. TUTAKUSIKILIZA NA KUFANYIA KAZI NA WEWE UWE UNAFATILIA KILA HATUA.. NA IKIBIDI PIA TUNAWEZA KUCHUKUA USHAURI TOKA KWAKO UNAOFAA... NTAMUOMBA MH. NDUNGAI AWEKE SAA 1:30 KUZUNGUMZA NA WABUNGE WOTE FULL CORUM.. KUWAKUMBUSHA WAJIBU WAO KWA TAIFA NA SIYO SERA ZA VYAMA VYAO... MUNGU LIBARIKI MAAFIKIANO BUNGE LETU/ MUNGU MBARIKI RAISI WETU NA WABUNGE WETU WATAKA MAENDELEO NA SIYO MALUMBANO / MUNGU IBARIKI TANZANIA YETU KWA AMANI NA MAENDELEO. UZALENDO / UAMINIFU / NA UTENDAJI HAKI PENYE HAKI NDICHO KITAKACHO TUKWAMUA .. BE GOOD AND PATRIOTIC... SAFARI TUNAITAMBUA NI NDEFU LAKINI TUMESHAIANZA NA JPJM... SISI TUKO NAE MIMI WEWE YEYE YULE NA WALE ... TUOMBE MUNGU KWENYE DOSARI TUTENGENEZEKWA NIA NJEMA NA UKWELI.... MUNGU ATULINDE NA KUTUBARIKI....JPJM ENDELEA NA HII KAZI NGUMU TULIYOKUPA...DUA ZET ZIKO NA WEWE....

    ReplyDelete
  4. Zitto tunafurahi unapokuwa unaweza kuona mambo ambayo sisi wengine hatuyaoni au kuyajua.. Je wewe kama mzalendo mkereketwa na haya... unachukua hatua gani zaidi ya kuyafikisha bungeni ili uendeleze sokomoko zinazoendelea na kupewa vichwa vya habari na media visivyo stahili.. Mimi kukuona wewe kuwa ungeweza chukua hatua katika sehemu husika kama vile TAKUKURU / POLISI / MWANASHERIA NA MUENDESHA MASHTAKA... Hawa watu hizi ndiyo Role zao ambao wanatambulika kisheria na wao kuwajibika katika hoja yeyote utakayo wapelekea ninaimani Kazi watalifanyia ili mradi imethibitika hivyo na Mabalozi wetu watachangilia ufatiliaji katika nchi husika na ikibidi tutafanya international arbitration agreed between our involved countries.. Zitto wacha bunge letu na wananchi kuwapa fikra za sivyo ndivyo... Magufuli ameona mianya na anaishughulikia.. lakini usidhani kwamba ni rahisi atamaliza kwa siku au mwezi.. anazo list za priority naomba uwe na imani hiyo.. wewe pia unaweza kumtembelea Mh Majaliwa mlango wake uko wazi. na atakusikiliza na kazi atayafanyia bila kuwawe katika njia unayoa mua wewe.. sisi sote tunataka kuiona Tanzania mpya ya maendeleo na siyo ya siasa nyingi.. japo mnataka kuleta siasa katika haya... ndugu zangu sivyo hivyo... Maendeleo ni ya watanzania na sivyo ya wafuasi wa vyama.. KARIBU tAKUKURU / KARIBU pOLUA NA TISI/ kARIBU OFFICE YA W/MKUU.. TUTAKUSIKILIZA NA KUFANYIA KAZI NA WEWE UWE UNAFATILIA KILA HATUA.. NA IKIBIDI PIA TUNAWEZA KUCHUKUA USHAURI TOKA KWAKO UNAOFAA... NTAMUOMBA MH. NDUNGAI AWEKE SAA 1:30 KUZUNGUMZA NA WABUNGE WOTE FULL CORUM.. KUWAKUMBUSHA WAJIBU WAO KWA TAIFA NA SIYO SERA ZA VYAMA VYAO... MUNGU LIBARIKI MAAFIKIANO BUNGE LETU/ MUNGU MBARIKI RAISI WETU NA WABUNGE WETU WATAKA MAENDELEO NA SIYO MALUMBANO / MUNGU IBARIKI TANZANIA YETU KWA AMANI NA MAENDELEO. UZALENDO / UAMINIFU / NA UTENDAJI HAKI PENYE HAKI NDICHO KITAKACHO TUKWAMUA .. BE GOOD AND PATRIOTIC... SAFARI TUNAITAMBUA NI NDEFU LAKINI TUMESHAIANZA NA JPJM... SISI TUKO NAE MIMI WEWE YEYE YULE NA WALE ... TUOMBE MUNGU KWENYE DOSARI TUTENGENEZEKWA NIA NJEMA NA UKWELI.... MUNGU ATULINDE NA KUTUBARIKI....JPJM ENDELEA NA HII KAZI NGUMU TULIYOKUPA...DUA ZET ZIKO NA WEWE....

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad