Apigwa Risasi na Kuuwawa na Majambazi Mbezi

Jana usiku yametokea mauwaji ya mtu mmoja mwanaume kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi katika Bar ya Kadabla iliyopo katikati ya Mbezi kwa Msuguli na Kibanda cha Mkaa.Mauwaji hayo yametokea kati ya majira ya saa tano usiku hadi saa saba usiku

Mashuhuda wa tukio katika eneo hilo wanasema marehemu alifika katika Bar hiyo ambayo amezoea kufika mara kwa mara anapokuwa anatoka kwenye mihangaiko yake maeneo ya K'koo,usiku wa jana alifika akiwa peke yake na kuegesha gari kisha kuanza kupoza koo.

Baada ya muda kupita,alimpigia mkewe ambaye wanaishi nae maeneo ya Mbezi Mwisho eneo la Tanesco njia ya kwenda Malamba Mawili,wito huo kwa mkewe ilikuwa kwa ajili ya kukaa wote ili waagize "kitimoto" na kuburudika pamoja.Katika ya burudani ya moja moto na mbili baridi huku kitimoto ikiwa inakaangwa jikoni kwa Mangi,walikuja watu wasiopungua wawili na kuanza kugongagonga gari lake,ilibidi aamke ili kujua kulikoni watu hao kugonga gari lake?

Baada ya maulizo hayo,wale jamaa wakamwambia wao wanataka pesa,wanajuwa ana pesa ndani ya gari,hivyo wanazitaka.Yakatokea mabishano na baadae jamaa wakampiga risasi mbele ya mke wake na kuchukua maisha yake huku wakitokomea na kiasi cha pesa kilichokuwepo.Kulizuka taharuki na watu kuacha vinywaji vyao na chakula juu ya meza na kutawanyika,hata waliokuwa "tungi" waliweza kukimbia bila kuyumba.

Msiba uko nyumbani kwa marehemu maeneo ya Mbezi Mwisho(Tanesco Maghorofani) njia ya kwenda Malamba Mawili.Bwana alitoa na bwana ametwaa,Jina lake lihimidiwe.

Polisi iamke na kutazama matukio haya ya uhalifu maana watu wanauwa wazi wazi na silaha za moto zimeenea hovyo hovyo.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mungu awaepushe na kiti moto. Kwani huyu jamaa angefanya maamuzi sahihi ya kwenda moja kwa moja nyumbani na kujipumzikia na familia yake pengine hii adha ya kuvamiwa na kuuwawa na majambazi isingemkuta. Anyways, Mungu aipe hii familia Nguvu katika kipindi hiki kigumu. Hii ndio wenzetu wanaiita "Being at the wrong place at the time" Case closed!! Ni bahati mbaya sana. Ni wakati mwingine sisi Watanzania inabidi tujifunze, hizi tabia za kushinda shinda kwenye Mabaa usiku wa manane sio kitu kizuri hata kidogo. Tujifunze kuwa tunarudi nyumbani mapema na kukaa na familia zetu. Kwani hii tabia ya kushinda shinda kwenye mabaa hata Mungu haimpendezi.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad