Bongo ina wasanii wengi sana, kati yao 90% hawajui muziki kifupi ni wabovu akiwemo Diamond ila wanapendwa kupita maelezo, na 10% wanajua muziki kifupi ni wakali akiwemo Rama dee na Steve wa RnB ila cha kushangaza hawapendwi(muziki wao).
Sasa nashindwa kuelewa inakuwaje?? Mfano huyu Diamond miziki yake ni ya kawaida tu lakini raia wanamshobokea vibaya sana, kila ngoma anayotoa inakuwa ni national anthem lakini nikisikiliza mi naona ni miziki tu ya kawaida ambayo hata kwenye flash au laptop au memory card yangu siwezi kuweka.
Sijajua watu ni kwamba hawajui muziki au ni nini tatizo au ni ufreemason na uganga wa kupumbaza watu?? Kama ni mganga basi ni kiboko aisee, nasema ukweli ngoma za jamaa ninazozikubali ni Nitarejea na kesho, basi!
Bado Sijajua watu Wanaupendea nini Muziki wa Diamond Platnumz
9
May 08, 2016
Tags
anatabia ya kuhonga mpaka media ili wamtangaze na nyimbo zake ziwe no1. hana lolote dumba ndo usiseme.
ReplyDeleteha ha ha na huko marekani kahonga?????? acheni wivu jamani. ngoma zake kali sana. sio kwa wabongo tu afrika mzima. kwani hizo tuzo anazopata ni wabongo tu ndio wanampigia kura????? acheni wivu wa kijinga. eti anaroga!!! nawewe karoge basi uwe maarufu
DeleteHapo umesem ukweli hata mimi sion ni nyimbo gan za Diamond zeny nawez pend isipokua nyimb mbili tu. Na sielew ni kwa nini wat wanapend et ngom kal. Na alipo kuja huk Sweden sikwend kweny show yake kwan nilion itakua kupotez mda wang wa bure, kwan jamaa hajui kuimb hata kidogo. Ila Kiba akija ao hawa Wanaume family hapo nitakwend kwan wat haw nawakubal sana.
ReplyDeleteMwenzio aliporudi kutoka Marekani alisema ana mpango wa kufanya Collabo na Kanye West kisa alipiga picha nae , tulicheka ile mbaya , huku USA tunavyomjuwa Kanye alivyo ,
Deletelakini mwache awazuge madinywa wa Bongo , kama issue ni Picha si yule
naniino lady C Wambura nani sijui ....si alipiga picha na marappa chungu nzima ? ufalla kitu kubaya sana ...
Wakati mwingine unawaza kina Mbaraka mwinshehe Mwaruka , Marijani mwana manyema ..... ah! Mungu awaweke pahala pema peponi .
Siku moja nilikuwa nasikiliza mziki wa Diamond " Ninywe pombe mpaka nilewe" Watu nao eti wanapenda musiki wa namna hiyo. Hakuna tena miziki, miziki yetu ya kale na nzuri imekufa!!
ReplyDeletepole sana wivu tu huna lolote.
Deletemaneno ya mkosaji haya!!!
Deletemtakufa msikini sana jitambueni mwenzenu anajitambua sana ndo maana anafanikiwa mtabakia vinywa wazi na kuanzika mambo ambayo hayana maana
ReplyDeletemtakufa msikini sana jitambueni mwenzenu anajitambua sana ndo maana anafanikiwa mtabakia vinywa wazi na kuanzika mambo ambayo hayana maana
ReplyDelete