BUNGE LIVE: Ushauri wa bure kabisa kwa vyama vya upinzani

Ushauri wangu kwa Wabunge wa Upinzani.

Waachane kupoteza muda kuvutana juu ya bunge kuwa laivu bali waangalie plan B .Kwa kuwa hata wafanyaje hiyo itakuwa hivyo kutokana na uchache wao ndani ya Bunge.

Plan B-wawafanyie kazi watu wao kwa kuisimamia Serikali vizuri katika maeneo yao ili yale matunda ndio iwe sera yao katika vyombo vya habari.
Mfano: Tumeona bajeti ya jimbo la kinondoni ni nzuri sana na kama itaenda kama ilivyopangwa basi utakuwa mfano nzuri na watu wataona umuhimu wa upinzani kuongoza jimbo.

Kama wataendelea kuvutana na serikali huku mambo yakiwa yanaenda pasipo kuona impacts za kugoma kwa wabunge wa upinzani basi serikali ambayo ipo chini ya CCM na huu moto wa mh rais serikali itazidi kujizolea sifa kwa kuwa wanacho kifanya wananchi wanakiona .

Ni upinzani kukaa na kujitathmini mapema sana bila ya hivyo watakuja kujitathmini wakati Mh rais yeye anasema jamani wananchi katika miaka yangu 5 nimefanya 1,2,3,4,5....naombeni tena mnipe miaka 5 nifanye 1,2,3,4,5...

Wakati huo wapinzani watabaki na mabomu (tuhuma za ufisadi mbalimbali) kwenye mikoba yasiyo na madhara ambayo wananchi wamechoka kuyasikia.

Siku hazigandi kama alivyoimba mwanamuziki mmoja maarufu nchini. Muda wa wao kufanya jambo la maana ndio huu.
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. UMEWASHAURI VIZURI SANA WASIKALIE LIVE MBONA WAO WANPOKAA VIKAO VYAO VYA NDANI HAWAONESHI LIVE KAMA WAPIGANIA HILO WAANZE KWANZA KUJIKATAA WAO KWA KUONYESHA VIKAIO VYA NDANI LIVE NDIPO TUJE BUNGE WAKAPIMWE AKILI

    ReplyDelete
  2. Kaka umesema kitu ha maana sana jamaa hawa hawakui wala kufikiria kitu cha maana, ndiyo maana hata sisi wananchi tumewachoka. Akili zao ni kuhakikisha wanavutana na serikali kuhusu kutangazwa bunge moja kwa moja,Lugumi,kuuzwa nyumba za serikali, kivuko cha Bagamoyo na nia ni kuhakikisha wanamkatisha tamaa Dr JPM. Sisi tuliua kuwa kuchaguliwa kwa Saed Kubenea na wengine upinzani umekufa kwa sababu hawa jamaa ni mivutano tu huku wananchi wakiendelea kupata shida.Tuliwashauri kuwa walishafanya kosa toka awali na kosa hilo litawaghalimu kwa miaka 15 ijayo kama watafanya mabadiliko sasa hivi kama hawafanya basi wasahau labda waanze upya. Opposition hawana strategies wamelala na kuangalia makosa ya serikali ambayo ni kidogo sasa wameanza hata kufufua mifupa ya wafu.

    ReplyDelete
  3. Labda hujaelewa.bunge kuwa live ni haki ya kila zmtanzania.hapa sikuungi mkono.pia mambo mengi yanavyoendeshwa na serikali hayafuati sheria za nchi.raisi no kiongozi wa ngazi ,a juu ssna.kitakachomfanya raisi ashinde ni kuwachagua mawaziri wenye upeo wa kazi, utendaji sagi wa kazi na ufuatiliaji wake.raisi ameingilia kazi nyingi za viongpzi aliowateua mwenyewe.Rasi anafanya kazi holela na za mitaani.humo kunawatu wake ambap amewaingilia kikazi.na hao watu wamechanganyikiwa na wana eoga.huwezi kuendesha nvhi kwa woga.kazi ya raisi ilimuwa kuhakikisha viongozi wake aliowachagua wanachapa kazi vipasavyo kwa kasi ansyoitaka.wengi watanzsnia hamjui mipaka ya kazi. Heshima ya cheo chako.kuna mwingiliano kikazi na hii haitakiwi.raisi ilibidi arudishe kwanza katiba ya wananchi ili iongoze kisheria.ingemsaidia sana katika tumbua anayoifanya. Nimemsikiliza ongea yake, ndio mafisadi wapo na wengi wao ni katika chama chake.majipu ni wanachama na biongoxi wote wakuu ndani ya chama hivho.kama kweli anania ya kutumbua aanze na vyombo vya sheria, polisi wanaoshirimiana na uongozi wa ccm ambao ni majipu mengi, wanajeshi ambao ni walinxi wakuu wa nchi ambao wametumika na wanatumika na chama chake.hapa ningemuona anaupeo wa hali ya juu ingemrahisishia mazi yake.lakini anania njema na upeo mdogo.hili linakuwa tatizo kiutawala.sheria za nchi hazijafuatwa wala kubireshwa.majaji, mahakimu, wapelelezi, mapolisi , hivi vyote vinabidi vitende haki, vifuate sheria na viwe nadhifu kwanza.wengi wetu watanzania pia tunaupeo mdogo.tuliendeshwa kwa muda mwingi bila uhuru wa mawazo na mchango kiserikali.tumelala na kutegemea viongozi wasio na uwezo wakijibabaisha na kuturudisha nyuma.tusingekuwa maskini namna hii na tusingehujumiwa na viongoxi dhaifu wexi, na wasio na uwezo na wadanganyifu.

    ReplyDelete
  4. We uko wapi???? Lakini kweli wapinzani wanaona haya mnayowaambia???
    Wacha wang'ang'ane na Bunge LIVE wakijizika na kuzidi kumpa point Rais kwani wananchi hatukuwachagua wabunge ili tuwaone Bungeni LIVE hapana bali tulitaka wakaziwakilishe kero zetu na mahitaji yetu kwa maisha bora siyo kuwaona kwenye TV
    Neno langu siku zote ni kwamba UPINZANI UNAKUFA KWANI HAWANA POINTI YOYOTE ILE NA BADO RAIS HAJAFANYA HATA robo ya ahadi zake bali anasawazisha uwanja na atakapoaanza kujenga wataduwa.
    HUU NDIO MWISHO WA UPINZANI hakuna kujipanga wala kujirekebisha kwani hawana issues zaidi ya BUNGE LIVE, LUGUMI,KUWATETEA WAHALIFU,

    ReplyDelete
  5. Nimeandika, lakini hachapishi. Shida gani..haya ni maoni.

    ReplyDelete
  6. Naona utoaji wa maoni una maslahi binafsi. Nionavyo Bunge live lina umuhimu wake, Rais wetu tumwombee wakati mwingine kama nyumba ni chafu huwezi kusubiri housegirl afangie wakati ugonjwa ukiingia ndani mtapata wote. Nafikiri mh Rais anaamua kuingilia kazi za watendaji wengine pindi anapoona madhara yakiachwa yanaweza kumdhuru hata yeye.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad