Chadema: Bunge la Sasa Kibogoyo Limeng'olewa Meno na Serikali

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dk Vincent Mashinji amesema kitendo cha Serikali ya Awamu ya Tano kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya Bunge ni sawa na kuling’oa meno bunge hilo.

Tofauti na mikutano miwili iliyopita ya Novemba 2015 na Januari/ Februari 2016, Serikali hii inayoongozwa na Rais John Magufuli, iliamua kufuta matangazo ya moja kwa moja ya Bunge la Bajeti lililoanza vikao vyake Aprili 19 kwa maelezo kwamba ni gharama kubwa kwa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC). Badala yake TBC huonyesha kipindi cha maswali na majibu pekee na hurekodi matangazo mengine na kurushwa katika kipindi cha ‘Leo katika Bunge’ saa nne usiku.

Suala hilo lilipingwa vikali na wabunge wa upinzani lakini uongozi wa Bunge ulitia chumvi kwenye kidonda baada ya kukataza vyombo vya habari kupiga picha za video, badala yake wanatakiwa kuchukua picha kutoka kwa televisheni ya Bunge.

Akizungumzia hali hiyo jana alipofanya ziara katika ofisi za gazeti hili zilizopo Tabata jijini Dar es Salaam, Dk Mashinji alisema kuwa huu ni mkakati maalum uliosukwa na CCM ili kuvibana vyama vya upinzani.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huo ndio mwisho wa upinzani,, kama ajenda yao ni kurusha Bunge Live wakati hata nchi tajiri Duniani nyingi zake hazina utatratibu ukiachilia mbali Tanzania.
    Ni kasi ya JPM inawafanya upinzani washindwe kuwa na pointi ya kuzungumzia si Bungeni wala wakitembelea mitambo ya magazeti au vituo vya TV
    Wapuuzi hawa wanata ati waonekane Bungeni Live wakiwa wanaburuzwa na polisi kutolewa nje makoti kuchanika.
    Jiungeni tu na CCM mnakaribishwa!!!!!

    ReplyDelete
  2. Wanasiasa mnapenda SIASA...NGOJENI WAKAYI WA KAMPENI..SISI TUMECHOKA KUSIKIA SIASA NA UVIVU..MAANA YAKE MIELEKEO YETU NI TOFAUTI MLETE MALUMBANO..SAMAHANI HATUKO TAYARI KWA HAYO... TUNATALA KUUONA NCHI INABADILOKIKA KWA MTANZANIA SIO SERA ZA VYAMA KWA UJUMLA..MADARAKA YANATAKA UZALENDO NA UADILIFU..PINDI UNASIFA HIZI UTAWEZA KUWA MIONGONI MWA WATENDAJI NA WACHAPA KAZI...TUMEKUSIKIA LAKINII HAITUSAIDII...SIASA SIASA SIASA TUMECHOKAAAAAAAA!!!!

    ReplyDelete
  3. Hivyo hai Wahariri WA magazeti..mtu akija na story utumbo au ya kukoda maadili ya anayo taka kusikia mtanzania huwa hamuutolee nje...au ndiyo uchochezi WA skendo na sokomoko

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndiyo manayake, Mhariri hachagui story ya wananchi na nchi.. kwa ajili Audience anayo taka iwafikie amwsha wazowesha.. Habari za dizaini hii.. na asipo leta kihivi hauzi gazeti.. Chochea / Controvesial / Skendo / na walio wengi wananunua halafu kibarazani wanadiscuss na ubishi utakuwepo the DAY is Gone Unproductive. Who loose the individual and the Nation as a whole... Tubadilike na mifumo yetuya Elimu tuipitie tena.. Kuokoa Vizazi.. Wahariri na Vyuo vyetu vya Journalism..Needs Genuine training for the benefit of the Nation ili tuweze kupiga hatua tunayo lenga ya Maendeleo kwa TAIFA...Mungu ibariki Tanzania yetu na watu wake.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad