Chadema Wabeza Utumbuaji Majipu wa Magufuli, Wadai Bora Kikwete

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk Vincent Mashinji ameponda mtindo wa utawala wa Rais John Magufuli wa utumbuaji wa majipu akisema umekosa dira na kinachoendelea ni utashi wa kisiasa na kukurupuka.

Kazi kubwa aliyoifanya Rais Magufuli tangu aingie madarakani, katika kipindi cha miezi sita sasa ni kubana matumizi ya fedha za umma kwa kufuta safari za nje za watumishi, kuzuia mikutano kufanyika mahotelini, kuhimiza mamlaka husika kukusanya kodi, kupambana na watumishi hewa, kuwasimamisha au kutengua uteuzi wa watendaji aliodai kuwa ni wazembe na walioshindwa kwenda na kasi yake pamoja na kuwashughulikia wala rushwa na wahujumu uchumi.

Katika namna inayoonekana ni kufuata upepo wa kisiasa, Rais Magufuli huwatumbua baadhi ya watendaji kwenye mikutano ya hadhara.

“Kuna vitu vingi vinafanyika lakini hatujui kipi ni kipi na wapi tunaelekea. Kuna mambo mengi yanafanyika, lakini hakuna hata mtu mmoja katika nchi hii anayejua Taifa hili lina mpango gani na linaelekea wapi,” Mashiji anakaririwa na gazeti la Mwananchi.

Huku akifananisha utawala wa Rais Magufuli na wa mtangulizi wake Jakaya Kikwete, Dk Mashinji alisema walau ahadi ya “Maisha bora kwa kila Mtanzania” ilikuwa inaeleweka hata kama haikutekelezeka.

“Rais Kikwete alitwambia Maisha bora kwa kila Mtanzania na tulijua maisha hayo yanapatikana kwa kupambana wenyewe na tulipambana. Lakini sasa hatujui tunaelekea wapi. Hapa kazi tu! Umemfukuza huyu kazi halafu nini kitaendelea? Keshaondoka kakuacha, unaajiri mwingine? Tunahitaji mtu wa kujibu hayo maswali. Nchi yote sasa inavurugwa. Halmashauri zinavurugwa,” alisema.

Katibu mkuu huyo alisema kwa sasa kila kitu kinavurugwa jambo ambalo ni hatari kwa mustakabali wa nchi na kwamba inaonekana wazi nchi inaelekea sehemu ambayo mbele kuna giza.

Akitoa mfano wa mfumo ulivyobadilika alisema hivi sasa wakurugenzi wa halmashauri wametangaziwa kusitisha mawakala wote wanaokusanya ushuru badala yake wakusanye wenyewe.

 “Hivi tujiulize halmashauri ina wafanyakazi wangapi ambao wana uwezo wa kukusanya mapato yake? Huku ni kudanganyana,” alisisitiza Dk Mashinji.

Hata hivyo, Dk Mashinji alisema hawapingi anachokifanya bali tofauti yao na Rais Magufuli ni namna ya kukabiliana na jambo.

“Sisi tunaamini katika mfumo na siyo mtu. Huwezi leo kuniambia meya anaiba Sh5 bilioni halafu chama kisijue. Kwa nini chama kisimwondolee udhamini kabla?” alihoji.

 “Anachofanya sasa ni kudhibiti na siyo kurekebisha mfumo. Rais Magufuli hana dhamana na Mungu, asipokuwepo sioni wa kuendeleza falsafa zake. Kwa nini kusiwe na mfumo madhubuti ambao upo kisheria na kila mmoja aujue na kuufuata?” alieleza.
Tags

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kweli nyie hamna shukurani kabisa. sasa kwenu jema lipi??? JK alikia mtaliii, hatuwaelewi wenzetu

    ReplyDelete
  2. Wavivu,waongo,mafisadi,wenye uchu wa madaraka na wengi wenye uovu ndio wanaopinga utendaji wa magufuli,sitashangaa kusikia na wewe ni mmoja kati hao,TUTAKUTUMBUA.

    ReplyDelete
  3. Hana akili kabisa nyang'au mkubwa huyo yeye na xhama chake cha CHADEMA ambao kazi zao ni kupinga kila lijalo. Huyo ni jipu kabisa.

    ReplyDelete
  4. Mbona hamzunguumzii mema ya rais wetu kipenzi,zaidi mwataka aonekane mbaya. Mwacheni jamani looooh

    ReplyDelete
  5. Tatizo lenu nyinyi hapo juu hajui sheria za nchi.watanzania ni watu wenye ufinyu wa kufikiri..hata wakiburutwa watakubali.cheo cha uraisi ni cheo kikuu cha kukiheshimu.hapa kina hotakiwa ni sheria wazi huru na ifuatwe .kusufi watu wajue mwenyekosa atachukuliwa sheria wazi atapelekwa mahakamani na kuchukuliwa hatua .kufukuzwa, kufungwa na kipa.badala yake raisi anachagua watu wa kuwatumbua akiacha vigogo waku wa sukari, akina Ridhiwani watoto wa kikwete na kesi ya kufunga mashine na polisi husika.anawaogopa.huko ndiko kulikoanzia matatizo yote haya.vigogo na watoto wao na vyombo vya umma.hivi na hawa ndio waliosababisha watu wengine wachini kuwaufuata.

    ReplyDelete
  6. Tuwasamehe mafyongo hawa.

    ReplyDelete
  7. Tatizo lenu nyinyi hapo juu hajui sheria za nchi.watanzania ni watu wenye ufinyu wa kufikiri..hata wakiburutwa watakubali.cheo cha uraisi ni cheo kikuu cha kukiheshimu.hapa kina hotakiwa ni sheria wazi huru na ifuatwe .kusufi watu wajue mwenyekosa atachukuliwa sheria wazi atapelekwa mahakamani na kuchukuliwa hatua .kufukuzwa, kufungwa na kipa.badala yake raisi anachagua watu wa kuwatumbua akiacha vigogo waku wa sukari, akina Ridhiwani watoto wa kikwete na kesi ya kufunga mashine na polisi husika.anawaogopa.huko ndiko kulikoanzia matatizo yote haya.vigogo na watoto wao na vyombo vya umma.hivi na hawa ndio waliosababisha watu wengine wachini kuwaufuata.

    ReplyDelete
  8. Wagonjwa wengine karibu na kufaa huongea utumbo tupu,, hivi hapo kweli kuna kitu ameongea??? na watu wa magazeti muwe wasomi kidogo siyo kutuhabarisha uppuzi kama huuu
    Upinzani sasa ni kama mgonjwa mahututi iteni ndugu na jamaa walio mbali!!!

    ReplyDelete
  9. Yaani bora kikwete kuliko Magufuli sasa hii kali kabisa,chadema wameishiwa cha kusema. Inaonyesha jinsi gani chadema walivyokumbatia viongozi wa hovyo.

    ReplyDelete
  10. Hivyo huyu Jamma Ni nani?? Mbona uchaguzi WA Laisi umesh kwisha siku nyingi. Sasa yeye anagombea nini??..Kama siyoo Laivu mbwana! Hata gazeti poa tuu..

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad