Diamond, Wizkid, Flavour Kutumbuiza Barclays Center, New York, July 22

Ni ukumbi wa ndani kwa ndani maarufu mno jijini New York, Marekani nyumbani kwa wasanii wakubwa wakiwemo Jay Z, Beyonce, Justin Bieber, Rihanna, Drake, taja kila msanii mkubwa wa Marekani, amewahi kutumbuiza hapo.

Na sasa Diamond, Wizkid na Flavour, watakuwa wasanii wa kwanza wanaofanyia muziki Afrika kuwahi kutumbuiza kwenye ukumbi huo. Mastaa hao watatumbuiza kwenye tamasha la muziki la One Africa July 22, 2016 kwenye ukumbi huo wenye uwezo wa kujaza watu 20,000.

“We are about to Make a History America!!!…. Platnumz Diamond with my Fellow African brothers and Sisters will be Shutting the Barclays Center Down! On the 22nd Jully 2016 in New York!…. 20k Seat Capacity!…Now make sure you tell your Friend to tell a Friend,” ameandika Diamond.


Barclays Center ni ukumbi unaotumika kwa shughuli mbalimbali na upo Brooklyn, New York City. Pia hutumika kama uwanja wa nyumbani wa timu ya kikapu ya Brooklyn Nets pamoja na New York Islanders ya National Hockey League.

Show ya kwanza kufanyika kwenye ukumbi huo ilikuwa ya Jay Z, September 28, 2012.
Tags

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Cha ajabu kitu gani ?
    Akapige hadi Ikulu ya USA

    ReplyDelete
    Replies
    1. HA HA HA BROVA DIAMOND. !!!!!!

      Delete
    2. mijitu minafiki na yenye wivu utayaona tu mbumbavu zako kwani kuandikwa kwa diamond kumekupunguzia nini?

      Delete
  2. Safi DIAMOND wewe uko juu ya wasanii wote E.Africa na watu waache kukulinganisha na msanii anayejulikana mwisho k/koo.

    ReplyDelete
  3. yuko juu kwa kuroga na kufitinisha wenzie ili asishuke. nyimbo zenyewe mbaya kazi kutafuta kiki kwa maa x wake. ops! This time atamuimba Irenny.

    ReplyDelete
    Replies
    1. HAYA MTAKALIAGA HAYO TU ANARONGA WAKATI ANAPIGA KAZI NA INAONEKANA NA KILA MTU. WABONGO BWANA!!!! WIVU UMEKUZIDI WEWE HUNA LOLOTE. POLE. DIAMOND WE PIGA KAZI ACHA WASEME MCHANA USIKU WANALALA

      Delete
    2. kama nakaona karoho kako kanavyodunda kwa wivu!!!!!!!!

      Delete
  4. Chukua 5 mtized popote ulipo

    ReplyDelete
  5. KULA TANO DIAMOND PEPERUSHA VEMA BENDERA YA TANZANIA!!!!

    ReplyDelete
  6. wenye wivu wajinyonge!!!! upo matawi saaana.

    ReplyDelete
  7. Biblia inasema asiyefanya kazi asile,mwanaume utakula kwa jasho,mwanamke utazaa kwa uchungu,Yesu nakuomba umbaliki DIamond kazi za mikono yake idumu ,umaarufu wake uongezeke,tangaza Nchi yako, ulimwenguni kote,Imana ikulinde chane.Beaty Semuguruka

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad