EDWARD Lowassa Achomoza Kamati Kuu ya CCM Dodoma..

Ukimya wa aliyekuwa mgombea wa Urais wa UKAWA,Edward Lowassa umezua mjadala kwenye mkutano wa Kamati Kuu ya CCM.Kikao cha Kamati Kuu kimefanyika jana hapa Dodoma. 

Mjadala ulianza pale Mwenyekiti Kikwete alipochagiza maelezo yake ya chama kuendelea kufanya maandalizi ya chaguzi zijazo na kutobweteka. Mwenyekiti alisema kuwa Lowassa bado ana uungwaji mkono na nguvu ya kisiasa na hutumia ukimya kujijenga zaidi.

Mwenyekiti alionya kuwa Lowassa hakufika mwisho na chama chapaswa kuutazama ukimya wake wa kuchangia na kutoa hoja juu ya Serikali ya Rais Magufuli kwa jicho la tatu. Wajumbe wote wa KK walikubaliana na Mwenyekiti Kikwete.

Wakati huohuo,Rais Magufuli ameaswa kuwa 'mpole kiasi' atakapoukwaa uenyekiti wa taifa wa CCM mnamo mwezi Juni mwaka huu. Imesemwa kuwa wanachama wa chama cha siasa hutendewa mambo kwa upole ili wabaki chamani na kukijenga chama. KK imeunga mkono hatua za Rais na Serikali yake kutumbua majipu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mnamwogopa Lowassa mnasababu.
    Hapa ukweli wajitokeza.
    Kunakitu Lowassa anakifahamu na mnakijua.
    Lakini hamuwezi kukigubika. Kiawaka moto kama Volcano.
    Mnamuunga mkono Magufuli sababu bado hajawatumbueni. Mnamweka sawa
    Ili mmbane asiwatumbue.
    Haya basi Wana CCM. Mnawachagua wale hawana sauti wanakondoo wenu.
    Mgiro arawafichieni ya Uingereza.

    ReplyDelete
  2. Udaku na speculation amabazo hazijengi. Mbona wakati CDM wanafanya mikutano Yao ulikuwa huupdate Na ulikuwa kwenye kikao. Aacha uzushi uwe unatoa Na source ya habari.

    ReplyDelete
  3. Ukimya wa edo hautushangazi, alishasema akishindwa ataenda kuchunga ng'ombe. Hata hivo hivi sasa yupo 'bize' na kesi ya 'mkwewe' anaye'nyea' ndoo segerea......HAPANA CHEZEIYA JPM

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad